https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    AFCON 2015: Congo Brazzaville Wapata Ushindi Wa Kwanza Tangu 1974

    Timu ya taifa ya Congo Brazzaville usiku wa kuamkia hii leo ilipata ushindi wake wa kwanza katika fainali za mataifa ya Afrika tangu mwaka 1974, baada ya kuishinda timu ya taifa ya Gabon katika mtanange wa mzunguuko wa pili wa kundi la kwanza.

    Congo Brazzaville walibahatika kupata ushindi huyo katika dakika ya 48, kupitia kwa kiungo wa klabu ya nchini Ufaransa Stade de Reims, Prince Oniangue.
    Ushindi huo unaipa nafasi timu ya Congo Brazzaville kufikiriwa kuwa sehemu ya timu ambazo huenda zikavuka katika hatua ya makundi, endapo itafanya vizuri katika mchezo wake wa mwisho dhidi ya Burkina Faso.
    Hali ya kufikiria katika muelekeo wa kufuzu, imejitokeza kutokana na matokeo ya mchezo wa kwanza wa kundi A, ambapo wenyeji Guinea ya Ikweta walishindwa kufurukuta mbele ya timu ya taifa ya Burkina Faso.
    Kwa mantiki hiyo sasa wenyeji Guinea Ikwete wamefikisha point mbili baada ya kupata matokeo ya sare katika michezo yao miwiwli waliyocheza, Burkina Faso wana point moja, Gabon pamoja na Congo Brazzaville wanamiliki point tatu kila mmoja.
    Fainali za mataifa ya Afrika za mwaka 2015 zinaendelea tena hii leo kwa michezo ya kundi la pili kuingia kwenye mzunguuko wa pili ambapo timu ya taifa ya Zambia itajitupa katika dimba la Nuevo de Ebebiyín, kucheza na timu ya Tunisia.
    Mchezo huo utakaounguruma katika mji wa Ebebiyín unatarajiwa kuwa na upinzani mkali kutokana na kila upande kutaka kuondoa aibu ya matokeo ya sare ya bao moja kwa moja waliyoyapata katika michezo ya mzunguuko wa kwanza.
    Mchezo huo utachezwa majira ya saa moja jioni kwa saa za Afrika mashariki.
    Mchezo wa pili ambao utachezwa mishale ya saa nne usiku kwa saa za Afrika ya mashariki utashuhudia timu ya taifa ya Congo ya Kabila ikipambana dhidi ya Cape Verde
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: AFCON 2015: Congo Brazzaville Wapata Ushindi Wa Kwanza Tangu 1974 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top