
Arsenal
wamemasajili kiungo Krystian Bielik kutoka klabu ya Legia Warsaw ya
Poland kwa pauni milioni 2.4. Bielik, 17, ambaye alifanya vipimo vya
afya wiki iliyopita, alihamia Legia akitokea Lech Poznan mwaka jana na
amecheza mara sita msimu huu. Arsenal wamesema mkataba huo "utakamilika
baada ya mchakato wa kawaida kumalizika". Bielik, ambaye aliwahi
kuichezea timu ya taifa ya Poland ya chini ya miaka 16, anaweza kucheza
kama kiungo wa kati, au beki wa kati.

