https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    Duh hatari sana :Picha na taarifa za uvamizi wa kituo cha Polisi cha Ikwiriri katika wilaya ya Rufiji mkoani Pwani


    Mwili wa mmoja wa Askari alievamiwa na kuchanwachanwa vibaya ukiwa Motchwari

    huyu ni mwingine askari alieuwawa katika tukio hili

    Majambazi yaliyojihamu kwa silaha yamevamia Kituo cha Polisi cha Ikwiriri, Rufiji mkoani Pwani na kuua askari wawili na kupora silaha zilizokuwepo kituoni hapo.

    Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo, huku askari wanaodaiwa kupotenza maisha ni Cop. Edgar aliyekatwa mapanga na WP Judith aliyepigwa risasi ubavuni upande wa kulia na kutokea upande wa kushoto.
    Hivi sasa hali ni tete katika eneo hilo na watu wamekusanyika huku polisi wakiongeza nguvu kusaka wauaji katika tukio la uvamizi, kituo cha polisi Ikwiriri, Rufiji, Pwani.
    Silaha zilizoporwa ni SMG 2, SAR 2, SHORTGUN 1, silaha 2 za mabomu ya machozi na risasi 60 za SMG.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: Duh hatari sana :Picha na taarifa za uvamizi wa kituo cha Polisi cha Ikwiriri katika wilaya ya Rufiji mkoani Pwani Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top