Labda litakuwa jambo jema sana
kwa mashabiki wa klabu ya AS Roma na Italia kumuona ‘ El Capitano’
Francesco Totti akiongeza walau msimu mmoja ili kujaribu kuvunja rekodi
iliyodumu kwa miaka 51 sasa katika kandanda la Italia. Nahodha huyo wa
Roma alifunga mara mbili na kuisaidia timu yake kupata alama moja katika
mchezo wa mahasimu wa Rome siku ya Jumapili.
Bao lake la
kwanza alifunga kwa mguu wa kulia akiwa ndani ya eneo la hatari
akimalizia pasi ya kiungo, Mholanzi, Kelvin Strochman. Lazio walikuwa
mbele kwa mabao mawili kufikia nusu ya mchezo katika uwanja wa Olympic,
Rome, lakini bao la Totti ambalo alifunga mara baada ya kuanza kwa
kipindi cha pili liliwarudisha mchezo vijana wa kocha, Rudi Garcia na ‘
King of Rome’ akafunga bao la kusawazisha katika dakika ya 63 huku
likiwa goli lake la 239 katika michezo 574.
Inashangaza
kiasi kumuona Totti, 38 akiendelea kufanya vizuri kwani ni mchezaji
ambaye alionekana kuandamwa na maumivu wakati mwingi wa uchezaji wake
lakini ameendelea kuyashinda maumivu kwa namna ya kuvutia. Wakati
mfungaji bora zaidi wa Italia, Silvio Piola alitumia michezo 619 kufunga
mabao 290 katika Serie A akiwa na klabu za Pro Vercelli, Torino,
Juventus na Novara kati ya miaka ya 1929-1954, Totti yuko klabuni Roma
kwa maisha yake yote.
Huyu ni kijana
halisi wa Rome – sehemu uliopo mji mtakatifu. Kwa mara ya kwanza Totti
aliichezea Roma, 28 Machi, 1993 baada ya kocha Vujadin Boskov kumpatia
nafasi katika mchezo wa kichapo cha mabao 2-0 ugenini kutoka kwa
Brescia.Amecheza katika klabu moja tu maishani.
KIUNGO MSHAMBULIAJI, MSHAMBULIAJI WA PILI AU WA KWANZA,
TOTTI alifikia
hatua ya kumchanganya aliyekuwa kocha wa I talia ‘ Azurri’, Dino Zofh
ambaye aliwahi kukiri hadharani kabla ya kuanza kwa michuano ya Uefa
Euro, 2000, Belgium & Holland kuwa hakufahamu nafasi gani ya
kumpanga Totti kutokana na uchezaji wake. Italia ikiwa na washambuliaji
wakali wenye uzoefu kama Roberto Baggio na Christian Vierri, Zofh
alifikiria kumuanzisha mshambulizi mmoja tu kati ya wakali hao ( baggio
& vierri) ili kumpatia nafasi kijana aliyekuwa na miaka 23, Totti.
Akiwa
mmaliziaji mahiri klabuni kwake, makocha wengi waliofanya kazi na Totti
katika timu ya Taifa walipendelea kumtumia mchezaji huyo kama
kiungo-mchezesha timu mwenye uwezo mkubwa wa kutengeneza/kujitengenezea
nafasi na kufunga mabao muhimu katika timu ya Italia. Akiwa ametoa pasi
za mwisho 147 hadi sasa, Totti alishiriki katika nusu ya mabao ya Azurri
katika michuano waliyoshuhudia wakipoteza siku ya mwisho mbele ya
Ufaransa kwa kulazwa mabao 2-1 katika mchezo wa fainali.
Totti alitajwa
kama mchezaji bora wa michuano hiyo ambayo wachezaji mahiri kama Luis
Figo, Raul Gonzalenz, Rui Costa, Patrick Kluivert, Dennis Bergikamp,
Zinedine Zidane, David Beckham na wengineo walishiriki.
Kumuona
akiendelea kufanya mambo makubwa akiwa na miaka 38 sasa ni jambo la
kupendeza sana kwa mchezaji huyo kipenzi cha Wataliano ambao wanaamini
ndiye namba kumi ( 10 ) bora kuwahi kutokea ulimwenguni. Mshindi huyo wa
taji la dunia, 2006 alipanga kustaafu soka mara baada ya kumalizika kwa
msimu uliopita. Huku klabu ikiweka wazi kuwa jezi namba 10 haitatumika
tena klabuni hapo kama heshima kwa mchezaji huyo.

