“Asamoah Gyan hakuwa fiti,
hakufanya mazoezi kama alivyostahili lakini unajua, yeye ni Asamoah
Gyan. Kama unaangalia takwimu, kama unaangalia tabia yake kwenye vyumba
vya kubadilishia nguo, utajua kuwa ni mchezaji mkubwa. Ni miongoni mwa
wachezaji wakubwa zaidi”.
“Hakuna wasiwasi juu ya hili.
Kwanza mara zote anafunga unapomhitaji na pili ni mzuri kwa kujenga
morali ya timu. Ni nahodha mzuri. Hebu fikiria kama angekuwepo kwenye
mechi ya kwanza, unadhani nini kingetokea”. Amesema kocha mkuu wa Ghana,
Avram Grant baada ya jana nyota huyo kuifungia bao moja Ghana
ikishinda 1-0 dhidi ya Algeria katika mechi ya pili ya kundi C.