Katika kuelekea mchezo muhimu unaoweza kuamua bingwa wa EPL msimu huu
– kati ya Chelsea vs Manchester City – huku City wakiwa nyuma kwa
pointi 5 dhidi ya viongozi wa ligi Chelsea. Kipigo chao cha nyumbani cha
2-0 kutoka Arsenal kilivunja rekodi yao ya kutopoteza mechi 14 katika
uwanja wa nyumbani. City hutajawazoea kupoteza mechi katika uwanja wao
wa nyumbani. Hata hivyo wana siku takribani 14 kabla hawajaenda Stamford
Bridge.

Lakini katika hizo wiki mbili bado Yaya Toure atakuwa hajarudi kutoka Afrika au mshambuliaji wao mpya Wilfred Bony. Kwa mara ya mwisho City kushinda mechi ya ligi bila uwepo wa Yaya Toure kwenye kikosi ilikuwa April 2014. Takwimu inayotoa ishara mbaya kwa timu aina ya City – hasa ukizingatia ukubwa wa mchezo dhidi ya Chelsea. Kupoteza mecho huo pale darajani kutamaanisha City wataachwa kwa pointi 8 na vijana wa Jose Mourinho.
Manchester City walimsajili Fernando ili kumpunguzia mzigo mkubwa Yaya Toure lakini mbrazil huyo hajatimiza majukumu yake hata kwa asilimia 50. Hachezi kama box-to-box midfielder na kuwa na wastani wa mabao 20 kwa msimu au kukaribia japo kidogo uwezo huo. Kukosekana kwa Toure kunaondoa mipango mingi katika safu ya kiungo ya timu hiyo. Hakuna mchezaji kwenye EPL mwenye wastani mzuri wa kupiga pasi kwa mechi kama Yaya Toure. Hata kama baadhi ya watu wanaweza kuwa na mashaka na uwezo wake kwenye kuzuia, lakini hakuna atakayepinga umuhimu wake kwa kikosi cha City. Ni injini ya timu.

Katika safu ya ushambuliaji Wilfred Bony alisajiliwa kumsaidia majeruhi Sergio Aguero, ambaye amekuwa na ‘pancha’ kila siku. Kwa maana hiyo michuano ya AFCON imekuja wakati mbaya, hata kama Bony alisajiliwa kwa mipango ya muda mrefu. Wangeweza kumtumia wikiendi iliyopita kama mbadala ya Aguero ambaye baada ya muda fulani alionekana amechoka katika mechi hiyo dhidi ya Gunners. Michuano ya AFCON imewadhoofisha City kwa kumchukua mchezaji wao muhimu kuliko wote kwenye kikosi pamoja na mchezaji wao mpya.

Je City watafanikiwa kukabiliana na ushindani uliopo mbele yao? Ili tutalijua katika wiki kadhaa zijazo. Lakini mtihani wa kwanza umeisha vibaya na mpaka mwisho wa mechi yao dhidi ya Chelsea tutaona ukubwa au udogo wa athari za kuwakosa Bony na Toure. Fernando anapewa mzigo mzito wa kuvaa viatu vya Toure, wakati Aguero ambaye bado anaonekana kusumbuliwa na majeruhi akiwa na presha ya kufunga magoli – Jovetic na Dzeko wamekuwa na ukame wa magoli msimu huu. Ni mtihani mgumu kwa timu yoyote kuziba pengo la kiungo tegemezi. Mpaka kufikia mwisho wa AFCON tutaona namna City watakavyoathiriwa na ratiba ya michuano hii.