Chukua kiasi cha karoti na apple kinachotosha kutengeneza juice kwa kiasi ulichokusudia. Anza kuandaa juisi yako kwa kuosha na kumenya karoti na apple kisha katakata katika vipande vidogo vinavyoweza kusagika kirahisi kwenye blenda. Saga mchanganyiko wako . Baada ya kupata mchanganyiko wa juice yako kamulia limao kwa ajili ya kuongeza ladha. Unaweza kuiweka kwenye friji ili ipate ubaridi . sukari haina ulazima sababu matunda yana sukari asilia.
FAIDA ZAKE MWILINI.
ina uwezo wa kutunza ngozi tunda la apple linaondoa uchafu kwenye ngozi na karoti nayo kwa kutumia kirutubisho cha beta-karotini chenye uwezo wa kutengeneza Vitamin A hulinda na kurejesha uhai katika ngozi na kuifanya ngozi kuwa nyororo. juice hii husafisha tumbo na kuondoa uchafu faida nyingine inasaidia ini lifanye kazi yake vizuri kwa kulainisha nyongo na kusaidia kuondoa uchafu.