ZAMBIA imelazimisha sare ya kufungana goli 1-1 na Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Congo (DR Congo) katika mechi ya kundi B ya mataiga
ya Afrika iliyopigwa kuanzia majira ya saa 1:00 usiku wa jana.
Bao la mapema la Given Singuluma (dakika ya 2′) liliwaamsha
mashabiki wa Chipolopolo, lakini katika dakika ya 66′ kipindi cha pili
Yannick Bolasie alisawazisha bao hilo.
Mechi ya pili iliyoanza majira ya saa 4:00 usiku, miamba ya soka kaskazini mwa Afrika, Tunia ilitoka sare ya 1-1 na Cape Verde.
Tunisia walikuwa wa kwanza kuandika bao katika dakika ya
70′ kupitia kwa Mohamed Ali Moncer, lakini dakika ya 78′ Cape Verde
walisawazisha kupitia kwa Heldon aliyefunga kwa mkwaju wa penalti.
Cape Verde, nchi inayotajwa kupata maendeleo makubwa ya
soka duniani katika kipindi cha miaka miwili au mitatu iliyopita
wameonesha ukomavu mkubwa katika mechi hiyo
MATOKEO YA MECHI ZA KUNDI B
| Africa Cup of Nations – Group BJanuary 18 | |||
|---|---|---|---|
| FT | Zambia | 1 – 1 | DR Congo |
| FT | Tunisia | 1 – 1 | Cape Verde |
Michuano hiyo itaendelea leo kwa mechi za mbili za kundi C kama inavyoonekana kwenye ratiba chini hapo chini;
| Africa Cup of Nations – Group CJanuary 19 | |||
|---|---|---|---|
| 19:00 | Ghana | ? – ? | Senegal |
| 22:00 | Algeria | ? – ? | South Africa |

