Imebainika
kuwa bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band
aka FFU-ughaibuni almaarufu viumbe wa ajabu Anunnaki Alien,inayoongoza
na mwanamuziki Ebrahim Makunja aka kamanda Ras Makunja,bendi hiyo
imejikuta ipo katika hali ya kukosa usingizi tena baada ya kutakiwa
kutumbuiza maomyesho zaidi katika msimu ujao wa joto.
Watayarishaji wa maonyesho makubwa
ya nje barani Ulaya wanashinikizwa na washabiki wao lazima waipandishe
jukwaani Ngoma Africa Band kutokana na mdundo wao Bongo dansi,maporota
hao baada kuwekwa roho juu na washabiki wao nao wamedhamiria
kuwapambanisha washabiki hao na bendi hiyo yenye makao yake nchini
Ujerumani,habari za uhakika zimetonya kuwa bendi hiyo imekubali kuenda
kutumbuiza katika nchi za Latvia na Austria na maonyesho mengine katika
msimu wa joto.
Habari
zimetonya kuwa hali hiyo inatokana na tabia za washabiki kushinikiza
bendi ya Ngoma Africa kuwepo katika ratiba ya mzunguko wa maonyesho
makubwa pamoja na wanamuziki hao kukosa muda wa kupumzika.
Hata
hivyo inasemekana kamanda Ras Makunja na kikosi chake wanauwezo wa aina
yake wa kuwamudu ratiba hiyo ngumu na kuwaburudisha washabiki wao
waliodata akili na jinamizi la muziki wa dansi wa bongo kule barani
ulaya.Ffu-Ughaibuni pia wanasikika online at www.ngoma-africa.com

