Msanii
anayetesa katika mziki wa kizazi kipya hapa nchini, Nassib
Abdul 'Diamond Platnumz' usiku wa jumamosi iliyopita alijikuta
katika wakati mgumu baada ya kuzomewa na mashabiki kwenye
viwanja vya Leaders Jijini Dar es Salaam.
Mbali
ya kuzomewa, Diamond pia alirushiwa chupa za maji ambazo
zilileta kadhia, lakini Diamond alionekana akiwahimiza madancer
wake wafanye kazi iliyowapeleka pale licha ya zomeazomea kuzidi
uwanjani.....
Msanii
huyo alipoona vitendo vya kutaka kumkwamisha asiimbe
vikiendelea, aliamua kuwamwagia fedha mashabiki hao, ndipo wakaacha
kuzomea na kuanza kugombea fedha hizo kisha kuanza
kumshangilia....
Baadhi
ya wadau walisikika wakidai, kundi hilo lililokuwa likimzomea
liko upande wa mmoja wa wasanii mahiri hapa nchini.Wasanii
wengine walioonja joto ya jiwe ni pamoja na Khamis Mwinjuma
'Mwana FA' na Ambwene Yesaya 'AY'.
Aidha,
baadhi ya mashabiki walilaani vikali tukio hilo la kumzomea
Diamond na kumrushia chupa za maji ambazo inadaiwa zilikuwa na
haja ndogo ndani yake.
Mashabiki
hao walisema tukio hilo halipendezi na linapaswa kukemewa na
kuwataka waratibu pamoja na jeshi la polisi kuzidisha ulinzi
katika matamasha makubwa kama hayo.
Hii
ni mara ya pili kwa Diamond kuzomewa,tukio la kwanza likiwa
kilele cha tamasha la Fiesta mwaka jana kwenye viwanja hivy