Kibano! Jamaa mmoja ambaye jina halikupatikana mara moja, amejikuta akinusa kifo baada ya kula kipigo ‘hevi’ wakati akifanya jaribio la wizi wa fedha kiasi cha shilingi laki 450,000 kupitia huduma za fedha kwa mitandao ya simu.
Akiomba kuachiwa baada ya kupewa kichapo kikali.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na Ijumaa Wikienda lilijiri wikiendi iliyopita maeneo ya Kijitonyama jijini Dar ambapo jamaa huyo alidaiwa kuingia kwenye duka moja akijifanya anataka kutoa shilingi laki nne na nusu (450,000/=) jambo lililomfanya wakala kumuonesha namba za kutolea kwa uchangamfu akijua ni mteja wa kawaida.
Dakika chache baadaye wakati wateja wengine wakiendelea kuhudumiwa, jamaa huyo alionesha meseji kuwa ametoa kiasi hicho cha fedha kupitia moja ya mitandao ya simu.
Wakala huyo alipoichukua meseji ya jamaa huyo ili kuhakikisha muamala wake alishangaa kuona meseji hiyo kuwa ni ya mtandao mwingine tofauti na alioutaja huku ikionesha imeandikwa au kutumwa na namba ya kawaida ya simu badala ya namba ya huduma hiyo ya mtandao husika.
Wakizidi kumshushia kichapo.
Wakala huyo, Maulid Vedasto alishangaa na kuamua kumshikilia jamaa
huyo akimuitia mwizi ndipo wananchi wenye hasira kali walipofika na
kumzingira wakimtaka atoe maelezo ya kutosha ambapo njemba huyo ilikiri
kutaka kuiba jambo lililoamsha hasira za watu walioamua kumshushia
kipigo hevi nusura afe.Akizungumza na Ijumaa Wikienda, wakala huyo alisema kuwa jamaa huyo alifika mara ya kwanza siku hiyo dukani kwake akitaka kutoa shilingi elfu sabini lakini alighairi na kurudi baada ya muda mfupi akitaka kufanya jaribio hilo la wizi.
Kichapo kikiendelea.
“Nilianza kumtilia shaka mara ya kwanza alipokuja na kujifanya
anataka kutoa fedha huku akiwa na wasiwasi na kila mara alipokuwa
akiwaona watu wengi ndipo alipokuwa akiniongelesha akijifanya ana haraka
ya kutoa fedha, akiona watu wachache anasubiri,” alisema wakala
huyo.Baada ya kunaswa jamaa huyo alipekuliwa kwenye simu yake ambapo
iligundulika kuwa kweli meseji hiyo haikuwa ya mtandao husika huku akiwa
hana salio.Katika kuhakikisha hilo, wakala huyo aliwapigia simu makao makuu ya mtandao huo na kupata taarifa kuwa hakuna salio la aina hiyo lililohamishwa kutoka kwenye simu ya jamaa huyo.Katika utetezi wake, jamaa huyo aliomba watu wasimuue kwa kuwa ni tamaa za kidunia zilimponza huku akikiri kufanya utapeli huo kwa kushirikiana na wenzake watatu ambapo wamefanikiwa kutapeli mawakala kibao jijini Dar.
“Jamani inatosha mlivyonipiga, naomba msiniue ni shetani tu amenipitia. Kweli nakiri kuwa nimewaibia mawakala wengi sana lakini nimekoma. Nipelekeni polisi msiniue,” alisema jamaa huyo ambaye alikuwa akivuja damu chapachapa kisha kupelekwa Kituo cha Polisi cha Kijitonyama ‘Mabatini’ kusubiri sheria kuchukua mkondo wake.