https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    Picha: Angalia Vurugu Na Silaha Za Hatari Zilizotumika Ktk Mchezo Wa Ghana Na Wenyeji

    Wachezaji wa Ghana wakielekea kwenye vyumba vya kubadilishia chini ya uangalizi mkali wa askari polisi.

    Baadhi ya vitu (Silaha) vilivyookotwa uwanjani mara baada ya hali ya utulivu kurejea.

    Helikopta ya Polisi iliyopelekwa uwanjani kutuliza ghasia za mashabiki.

    Mmoja wa mashabiki aliebainika kuwa sehemu ya walioanzisha fujo akiwa amebebwa na kikosi cha usalama cha uwanja wa Malabo.

    Michirizi ya damu iliyoganda katika mbao za matangazo ambazo huwekwa pembezoni mwa uwanja.

    Wachezaji wa Equatorial Guinea wakijaribu kukabiliana na matukio ya kurushiwa chupa za maji walipokua wakijaribu kuelekea katika vyumba vya kubadilishia.

    Askari wa usalama wakijaribu kuwatoa mashabiki wastaarabu uwanjani kwa hali ya amani.

    Chupa za maji zikionekana pembezoni mwa sehemu ya kuchezea ua uwanja wa Malabo.

    Baadhi ya waandishi wa habari wakitafakari huku wengine wakisaka mbinu za kujizuia na hatari.

    Mashabiki wakijaribu kujiokoa baada ya askari wa usalama kupiga mabomu ya machozi.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: Picha: Angalia Vurugu Na Silaha Za Hatari Zilizotumika Ktk Mchezo Wa Ghana Na Wenyeji Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top