SHIRIKA
la Ndege la Precision linatarajia kuuza baadhi ya ndege zake na
kubakiza ndege sita kupunguza mzigo wa madeni yanayoikabili Kampuni hiyo
kwa sasa.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa shirika hilo, Michael Shirima alisema Dar es
Salaam jana kuwa hatua hiyo imefikiwa kutokana na uchakavu wa ndege hizo
na hali ya uchumi wa kampuni.
“Kampuni
iko katika mazungumzo na mwekezaji ili kukamilisha makubaliano ya
kununua ndege zenye madeni na kisha kuzikodisha kwa kampuni nyingine…
makubaliano haya yanatarajiwa kufikiwa mwishoni mwa robo ya kwanza ya
mwaka huu,” alisema Shirima.
Alisema
pamoja na kufikia hatua hiyo kampuni haijakata tamaa kwa kuweka jitihada
ya kutafuta mtaji mkubwa kupitia kwa wanahisa wa sasa au wawekezaji
wasio wanahisa.
Awali
akiitoa taarifa katika mkutano mkuu wa mwaka wa Tatu wa wanahisa,
Shirima alisema mazingira ya biashara yalikuwa na ushindani huku kukiwa
na hofu juu ya usalama duniani kote.
Pia
alisema thamani ya fedha za kigeni hususan Dola ya Marekani imeendelea
kukua ikilinganisha na shilingi ya Tanzania hivyo kusababisha akiba
hafifu ya fedha za kigeni na hasara kwa biashara ambazo matumizi yake
mengi