Kila mmoja atakubaliana na mimi kwamba mahusiano baina ya wapendanao kwa
kawaida yanakusudia kuwa ya upendo, maelewano, kuaminiana na urafiki wa
hali ya juu ingawa hali halisi siyo hiyo katika uhusiano wa wengi.
Wengi wetu wameumizwa kwa mapenzi. Inawezekana mara moja au nyingi na
hasa kutokana na tatizo la uaminifu katika mahusiano yao.
Zifuatazo nia alama zitakazokusaidia kuwa macho mara utakapoona mazingira ya kufanana nazo yanatokea katika uhusiano wenu.
Wengine wanaondoa milio katika simu zao wakati haikuwa kawaida yao, kuwe siri (password) ngumu hadi mwenyewe anashindwa kuikumbuka, wako ambao simu zao zikipigwa hawawezi kupokea na kuongea kwa uhuru kama kawaida, ataondoka na kujitenga pembeni akijifanya anaongea kiuaminifu kabisa.
Zifuatazo nia alama zitakazokusaidia kuwa macho mara utakapoona mazingira ya kufanana nazo yanatokea katika uhusiano wenu.
1.Kuongezeka ghafla kwa hali ya kujipenda.
Yawezekana mpenzi wako alikuwa amezoea kuvaa kawaida, hapa simaanishi kutopendeza na wewe ulikuwa umemzoea katika halifulani ya mavazi au mitindo mara ghafla anabadilika na kuwa mtanashati zaidi ana badilisha mavazi, anapenda mavazi ya garama, labda alikuwa hatumii manukato lakini gafla anaanza kupenda manukato, anajijali zaidi ya kawaida yake kiasi ambacho hukumzoea. Katika hali hii jaribu kuwa macho zaidi kufahamu nini kilicho sababisha mabadiliko hayo..2.Kuanza kuchelewa kutoka kazini mara kwa mara.
Sio kwamba kila mtu anapochelewa kutoka kazini basi anakuwa sio mwaminifu, lakini zaidi ya asilimia 75 (kutoka kwenye tafiti) ya ambao wamekuwa na mahusiano nje wamekuwa wakitoa visingizio vinavyohusiana na kazi, vikao, mikutano na safari za kikazi, yamkini wewe ni shahidi wa hili.3.Anapenda kutembea na mipira ya kinga mara kwa mara (kondomu)
Inashangaza mara nyingine kusikia mpenzi mmoja ana tabia ya kubeba kondomu kwenye pochi yake au mfukoni kwa kisingizio kuwa anajali cha kushangaza zaidi unakuta yuko katika mahusiano na mkewe au mumewe.4.Mazingira tatanishi ya simu:
Gafla simu zinaanza kumiminika mpaka mida ya usiku. Yamkini pia alikuwa yuko huru hata simu yake inapolia waweza ichukua na kumpatia lakini gafla anakuwa na hofu kubwa na kuificha simu yake, nimeongea na wengine ambao wanakwenda na simu hadi bafuni isije ikasikika.Wengine wanaondoa milio katika simu zao wakati haikuwa kawaida yao, kuwe siri (password) ngumu hadi mwenyewe anashindwa kuikumbuka, wako ambao simu zao zikipigwa hawawezi kupokea na kuongea kwa uhuru kama kawaida, ataondoka na kujitenga pembeni akijifanya anaongea kiuaminifu kabisa.