Gardner
G Habash na Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jay D’ siku ya harusi
yao
BAADA
ya wiki iliyopita aliyekuwa mke wa mtangazaji wa kituo cha radio cha EFM,
Gardner G Habash, mwanamuziki Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jay D’ kumwaga sababu
za kuachana na mumewe huyo, mkali huyo wa kutangaza ameibuka na kusema
amechukizwa na maneno
yaliyotolewa na
aliyekuwa mwandani wake huyo huku akidai anamuachia Mungu.
Ishu
hiyo iliyopata nafasi kwenye vyombo mbalimbali vya habari, ilitokana na Jide
kuwapa watu nafasi mashabiki wake kumuuliza maswali katika mtandao wa kijamii,
ambapo asilimia kubwa walitaka kujua kama kweli ameachana na mume wake au
la.
Magazeti
Pendwa kutoka Global Publishers yakaamua kumtafuta Gardner ili aweke bayana juu
ya suala la ndoa yao kutokana na mwanamuziki huyo kuweka wazi kwamba tayari ndoa
yao ilikwishasambaratika.
“Alichokisema
na ulichokisikia ndiyo ukweli wenyewe. Hakuna ndoa tena, tumekwishaachana na
kila mmoja kuchukua kilicho chake. Ila kila kitu namwachia Mungu na wala sina
kinyongo naye,” alisema Gardner.
Siku
chache zilizopita mwanamuziki Jide alifunguka kwamba hakutaka tena kuendelea
kuishi na mume wake kutokana na tabia mbaya alizokuwa nazo mwanamume huyo, hali
iliyomfanya kuishi pasipo kuwa na furaha katika kipindi kirefu cha ndoa
yao.
Akifunguka
zaidi, Jide alisema kwamba alichoshwa na tabia hizo ambazo alipobanwa zaidi ili
aziweke wazi tabia hizo, alisema kwamba mwanamume huyo alikuwa na tabia ya
kuwashikashika wanawake kila alipokuwa jukwaani
akiimba.
Alipenda
kuwatongoza wanawake wengi tu ambapo kuna siku alimkuta akimshikashika mapaja
mwanamke ndani ya mghahawa wake, na alipomuuliza, alikiri kufanya hivyo na
kuomba msamaha.
Wawili hao walifunga ndoa Mei 14, 2005, jijini Dar es Salaam ambapo mpaka wanaachana, hawakubahatika kupata mtoto.
Wawili hao walifunga ndoa Mei 14, 2005, jijini Dar es Salaam ambapo mpaka wanaachana, hawakubahatika kupata mtoto.