Mshambuliaji
Machachari wa timu ya Ndanda,Masoud Ally akitoa pasi maridadi kabisa
mbele ya beki wa timu ya Yanga,Juma Abdul wakati wa mtanange wa ligi kuu
Tanzania Bara,uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar
es Salaam.Mechi hiyo imemalizika kwa suluhu ya 0-0.
Mrisho
Ngassa wa Yanga akiondoka na mpira huku akifuatwa na Beki wa
Ndanda,Paul Ngalema wakati wakati wa mtanange wa ligi kuu Tanzania
Bara,uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.Mechi hiyo imemalizika kwa suluhu ya 0-0.
Nyanda wa timu ya Yanga,Ally Mustafa akiwa makini kulilinda lango lake.
Mshambuliaji
wa timu ya Ndanda,Omega Seme akiangalia namna ya kumtoka Beki wa
Yanga,Oscar Joshua mtanange wa ligi kuu Tanzania Bara,uliomalizika hivi
punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Mechi hiyo imemalizika
kwa suluhu ya 0-0.
Beki
Hasifiwi: Beki wa timu ya Yanga,Rajab Zahir akiruka juu kuondoa hatari
iliyokuwa ikielekea langoni kwao katika mtanange wa ligi kuu Tanzania
Bara,uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.Mechi hiyo imemalizika kwa suluhu ya 0-0.
Beki wa timu ya Yanga,Rajab Zahir akiwania mpira na Jacob Massawe wa Ndanda.
Nadir Haroub wa Yanga akijaribu kuondosha hatari ilikuwa langoni kwake.
Dan Mrwanda wa Yanga akitafuta namna ya kumtoka beki wa Ndanda,Paul Ngalema.
Hapiti
mtu hapa: ni kama anaonekana kusema beki wa timu ya Ndanda,Paul
Ngalema wakati akimdhibiti Mshambuliaji wa Yanga,Simon Msuva.
ajali kazini.
Hatariiiii paleee....... daaahh.... wanakosa goli Yanga hapaaa....
Kocha wa Timu ya Yanga,Hans Van Der Pluijm akifanyiwa mahojiano na Mtangazaji wa Michezo wa Radio Clouds,Issa Maeda.
Chombo kiko tayari kwa kazi.
Wadau uwanjani.
Washabiki wa timu ya Ndanda wakiishangilia timu yao.