Watu wengi wamekuwa wakiniuliza kuhusu siku ambayo nitaongelea mada ya leo. Pengine ni kutokana na uzoefu nilionao kutokana na kuwa na salon & beauty spa na hivyo kuwa nimeshakutana na watu wengi wenye aina mbalimbali za nywele nk.
Ukweli ni kwamba nina uzoefu. Ukiachilia mbali kuwa na salon & beauty spa, mimi mwenyewe nipo “obsessed” na nywele zangu. Naweza kusema nimeshakuwa na nywele za kila aina.Kuanzia weaving,braids,wigs, relaxer nk. Kitu ambacho nilikuwa sijawahi kukifanya (at least tangu nilipokuwa msichana) ni kuziacha natural.
Mwaka juzi niliamua kuzipunguza (kuzikata) na kubakia natural. Ni kitu ambacho namshauri kila mtu ajaribu kukipitia. Najua wengi wetu mnaogopa. Lakini siku hizi ukiangalia kundi la wanawake 10 utakuta 9 wametumia extensions. Kwa hiyo nywele zao halisi (natural hair) zinaweza kuwa ndani na zikawa poa tu.
Kabla sijaanza kuzungumzia mahitaji ya nywele, ni muhimu kujua una aina gani za nywele. Ukijua utaweza kumudu vizuri zaidi mahitaji ya nywele zako. Aina za nywele tofauti zina mahitaji tofauti. Kuna ambazo zinahitaji kupakwa mafuta kila siku na kuna ambazo hazihitaji. Kuna ambazo zinahitaji “treatment” mara kwa mara. Kuna ambazo zinaweza kudumu kwa muda mrefu kabla ya kuhitaji kazi ya ziada.
Leo nitaanza kwanza na aina za nywele kwa juu juu tu bila kuingia ndani sana. Kuna siku nitaandika kwa undani zaidi kuhusu aina za nywele.
Picha hiyo hapo juu inaweza kukusaidia kujua aina za nywele ulizonazo. Njia nyepesi ya kujua aina ya nywele ulizonazo ni zikiwa zimeloa(wet). Zinapoanza kujikunja ndipo utajua aina za nywele ulizonazo. Picha ya chini (flat ironed) inaonyesha nywele zako zikiwa zimewekwa relaxer.
Kama nilivyogusia hapo juu, nilipoamua kuacha nywele zangu kuwa natural, kuna feeling fulani ambayo hata siwezi kuielezea. Unahisi kuwa huru kuliko kawaida. Ila usidhani ilikuwa rahisi kukubali kujaribu natural hair. Lakini baada ya kujaribu sijui kama naweza kurudi nyuma. Nikitamani relaxer, nina wigs za kila aina. Nazivaa kutegemea na mood.
Kama kichwa cha habari kinavyosema, sasa nianze kuongelea utunzaji wa nywele. Hizi hapa ni hatua ambazo mimi binafsi nazitumia ili kukuza na kutunza nywele.
Kuosha nywele.
Jambo la kwanza muhimu ni kuosha nywele zako kwa kutumia shampoo nzuri. Hapa nitazungumzia kidogo salons. Salon nyingi hawatumii shampoo zinazotakiwa kwenye nywele. Nyingine hata sio shampoo kabisa. Au kama ni shampoo zingine huwa zimechanganywa na maji (we’all know why,right?). Ushauri wangu; kama unaweza nenda na shampoo yako. Kama huwezi kwenda na shampoo yako jaribu kumuuliza hair dresser wako anatumia shampoo gani kisha i-google au itafute na kuichunguza kwanza. (Sorry Salon Owners)
Kusafisha nywele kunasaidia ngozi yako ya kichwa kupata hewa na pia kuzipa nafasi nywele kuota au kukua. Ingawa wataalamu mbalimbali wa nywele wanatofautiana kuhusu mara ngapi uoshe nywele zako, wengi wanakubaliana kwamba nywele zinatakiwa kuoshwa mara mbili kwa wiki -na co- wash na mara mbili kwa mwezi kwa shampoo.
Mimi kwa mapenzi yangu ya kuosha nywele hususani sasa na nywele natural, huziosha mara mbili kwa wiki na co wash na mara moja kwa mwezi na shampoo. Co-wash na shampoo wash zina tofauti gani? Tofauti ni kwamba tunaposema co-wash ni kuosha nywele zako kwa kutumia Conditioner tu bila shampoo. Shampoo wash ni kutumia shampoo ambayo ni sabuni.
Shampoo nyingi zina kitu kinaitwa sulfate. Kuna wengine inawakata sana nywele. Kwa hiyo utaona kwamba ingawa shampoo inatakatisha nywele/kichwa vizuri zaidi, ina madhara yake. Ndio maana inashauriwa kuosha kwa Co-wash zaidi hususani kwa watu wenye natural hair.
Nilipoanza kuacha nywele zangu kuwa natural, zilikuwa zinakatika (breakout) na hazikuwa healthy kama sasa. Nilitumia Carol’s Daughter products ambazo zilinisaidia.
Kila majira ya joto nazitumia tena(Mara nyingi nywele zangu zikipoteza muelekeo nakimbilia hizi products.)
Lakini kuna aina nyingi za shampoo na Co- wash nimetumia na naamini ni nzuri sana
Kwenye picha nimekuwekea aina 4 ambazo
nimetumia na naweza kuhakikisha ni nzuri. Mbili za mwanzo ni shampoo,
na mbili za mwisho ni Co-wash. Unaweza pata hizi products kwenye maduka
ya urembo au unaweza ingia amazon ku order online.
Conditioning
Conditioning ni muhimu sana wakati wowote
unapoosha nywele. Hata unapofanya co-wash, lazima utumie deep
conditioning. Hii inafanya nywele zako zisikakamae au kuwa kavu kupita
kiasi. Pia inasaidia kuzifanya nywele kuwa na nguvu na hivyo kupunguza
kukatika.
Pia ni muhimu sana kwa wale wanaopaka nywele
rangi au wanaotumia moto (dryer). Mimi mara nyingi nafanya deeep
conditioning angalau mara moja kwa mwezi. Hata hivyo,natumia
conditioner/conditioning kila nikiosha nywele.
Hizi mbili ndizo ninazozitumia zaidi.
Cholestrol kila nikiosha na co-wash na Shea Moisture kila nikitumia
shampoo.(nafanya treatment) Siri kubwa sana kuhusu conditioning nywele
zako ni leave- in- conditioner. Hiki ni kitu wengi sana wanasahau, na
wanafikiria labda kwasababu wanapaka tu wanapomaliza kuosha nywele
inatosha.
ukitaka kuwa na nywele ambazo zinaweza kuwa
balanced na kuzimudu, ni leave in conditioner. Utaona tofauti kati ya
nywele inayotumia leave in conditioner na ambayo haitumii hususani
wakati wa joto.
Nunua yako ambayo uwe unaweka kila asubuhi
ukiamka kabla hujaweka kitu chochote kichwani , baada ya week utaona
tofauti za nywele zako. Hii ndio ninayotumia kwa sasa. Zipo nyingine
nyingi.
Chache kati ya ambazo nimetumia na ni nzuri.
Detangle/Kuziachanisha Au Kuzichana
Kwa nywele zetu sisi, lazima
uzichambue/kuzichana. Zina tabia ya kujikusanya pamoja. Muhimu ni kujua
aina ya nywele ulizonazo. Ila kuwa makini kidogo; wakati unazi-detangle
nywele zako hakikisha sio kavu ili zisikatike.
Kwa uzoefu wangu, fanya hivyo baada ya
kuweka conditioner(mara moja kwa wiki). Tumia vidole badala ya chanuo.
Wakati mwingine huwa naacha ile natural curl ya nywele zangu. Hapo
utajua pia afya au ubora wa nywele zako.
Mbali ya vidole vifaa hivi vinaweza kusaidia. Lakini lazima ujue aina ya nywele zako kujua ipi inakufaa zaidi.
Moisturizer/Vilainishi Vya Nywele
Hakikisha unatumia moisturizer kila siku.
Mimi nafanya kila siku kwasababu nywele zangu ni kavu. Wengine hawafanyi
kila siku. Inategemea na aina za nywele ulizonazo. Wakati wa kuweka
moisturizer,hakikisha unapaka kila mahali haswa kwenye ncha za nywele
zako(split ends). Mara nyingi huwa tunazisahau zile za juu. Badala yake
wengi tunapaka zaidi kwenye ngozi ya kichwa tu. Ndio maana huwa
inasisitizwa kuzikata zile split ends kwa sababu huwa zimekauka na
dhaifu.
Mimi hupenda ku-moisturize nywele zangu
usiku wakati nakwenda kulala. Naamini usiku ndio wakati kila kitu
kinafanya kazi. Hii Almond Milk ya Carol’s Daughter ndio hutumia. Lakini kuna Moisturizer ambazo natumia mara kwa mara nazo ni Shear Moisture Curl&Style, T44z na Mizani moisture infusion
Hizi products unaweza zipata kwenye maduka ya nywele, au kama wewe ni wa on line angalia Ebay. Kwa Tanzania T444 zinapatikana 8020fashion
OILS/MAFUTA
Kuna aina nyingi za mafuta ya nywele. Kila
mmoja anadai kwamba yake ndio bora zaidi. Ushauri ninaoweza kukupa hapa
ni kwamba kwa sababu nywele zina tabia ya kubadilika(kuna sababu nyingi)
huna budi kutumia mafuta kwendana na aina ya nywele zako na pia
majira/hali ya hewa.
Ukitembea kwenye maduka ya vitu vya nywele
utaona aina mbalimbali za mafuta na maelezo kuhusu yanachosaidia nk. Kwa
upande wangu natumia zaidi Black Castrol, Jojoba Oil na Argan Oil.
Nazibadilisha tu kutokana na matakwa ya nywele.
Kuna aina nyingi ya haya mafuta, hakikisha tu hayajachakachuliwa.
Kutunza nywele yako kuna mengi sana ya
kujifunza.Kwa leo ntaishia hapa. Siku za karibuni nitaandika zaidi.
Natumaini itamsaidia mtu hususani wale ambao wanaingia kwenye natural
hair kutoka kwenye ulimwengu wa nywele za dawa,relaxers nk.
Hata hivyo hatua hizi unaweza kuzifuata hata
kama umeweka nywele zako dawa. Kwa wale mlioweka dawa,msikose hata mara
moja kuacha treatment,conditioner na moisturizer
0 comments:
Post a Comment