MBUNGE wa
viti maalum Mkoa wa Tanga, Amina Mwidau (CUF) ndiye Mwenyekiti mpya wa
Kamati ya PAC baada ya aliyekuwa mwenyekiti wake, Zitto Kabwe kung'atuka
kwenye nafasi yake ya ubunge.
"Nimefanya
kazi na Amina tangu mwaka 2010 tulipokuwa kamati ya POAC na nina imani,
kwa ushirikiano mkubwa wa Makamu Mwenyekiti ndugu Deo Filikunjombe
wataendeleza kazi tuliyoianza ya kujenga mfumo madhubuti wa Uwajibikaji
nchini kwetu" aliandika Zitto Kabwe.

