Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akipata maelezo ya mradi wa Maji
Taka katika Manispaa ya Sumbawanga kutoka kwa Ofisa Uhusiano wa Mamlaka
ya Maji Safi na Maji Taka Sumbawanga (SUWASA) Ndugu Zakaria Ngunda
alipofika kutembelea mradi huo tarehe 19/03/2015. Ujenzi wa mradi wa
Maji Taka umeshakamilika na kinachosubiriwa hivi sasa ni magari matatu
kwa ajili ya kuzolea taka za vyooni zitakazomwagwa katika mtambo huo
ili uanze kufanya kazi. Miradi yote mikubwa ya Maji Safi na Maji Taka
Mjini Sumbawanga inagharimu zaidi ya fedha za Kitanzania shilingi
bilioni 30.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na Wakandarasi
wanaojenga mradi Maji Safi na Maji Taka Mjini Sumbawanga ambao ni Techno
Fab na Mkandarasi mshauri GKW ambapo amewataka kuongeza kasi kumaliza
mradi huo ambao upo nyuma ya wakati. Amemuagiza Mkandarasi anaejenga
kukamilisha ujenzi huo kwa kipindi cha miezi miwili ijayo licha ya
kuomba kuongezewa muda wa miezi sita ili aweze kukamilisha kazi hiyo.
Alisema
kuwa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ni lazima uende na wakati
kuhakikisha huduma muhimu zinawafikia wananchi kwa wakati na hivyo
kupisha malalamiko ya wananchi kwa Serikali yao. Kwa upande mwingine
ameuagiza uongozi wa Maji Safi na Maji Taka Mjini Sumbawanga kumfikishia
taarifa za Mkandarasi Herken Builders Ltd aliyojenga mradi wa maji wa
visima nane na "pumps" ambazo hazifanyi kazi aweze kumchukulia hatua
stakihi ikiwepo kumuandikia barua kuwa hastahiki kufanya kazi katika
Mkoa wake wa Rukwa.
Mradi wa Bwawa la kuchujia Maji Taka Mjini Sumbawanga ukiwa umekamilika.
Sehemu ya Bwawa hilo.
Sehemu ya Mradi wa Maji Safi ambao ni Chujio la kuchuja Maji Safi kabla ya kwenda kwa walaji.
Sehemu ya Mradi wa Maji Safi.
Picha
nyuma ni sehemu pia ya ujenzi wa mradi mkubwa wa Maji Safi unaoendelea
katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga.(Na Hamza Temba - Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa Rukwa)








