https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    Hii ndio miji 9 salama zaidi kuendesha baiskeli duniani..

    big_thumb_92c6b6522f4508d7381a20d28edea6ef
    Katikati ya Jiji Dar es Salaam ni mfano mzuri kwamba japo watu wengi wanatumia magari na pikipiki au bajaji, lakini wapo pia ambao utakutana nao wakitumia usafiri wa baiskeli.. sasa
    mtu wangu hiyo sio BONGO pekeake ambapo watu wanaingia na baiskeli katikati ya miji na kuendelea na dili zao kama kawaida.
    Hapa nimekutana na hii record ambayo imetoka mwezi huu MARCH 2015, unajua miji au majiji ambayo yametajwa duniani kwamba ndio salama zaidi kwa kuendesha baiskeli.
    .
    No.1: Amsterdan, Netherlands. Miundombinu za mji huu zinafanya zaidi ya 38% ya watu wanaoingia town wanaingia kwa usafiri wa baiskeli.
    .
    No.2: Copenhagen, Denmark. Wao pia wana barabara nzuri kabisa pembeni ya barabara za magari ambazo wanatumia waenda kwa miguu na waendesha baiskeli. 36% ya watu wanaoenda shuleni, maofisini kwingineko wanatumia zaidi baiskeli.
    .
    No.3: Utrecht, Netherlands. Record inaonesha 33% ya watu wanatumia baiskeli kwenye safari zao za kila siku, wakati 19% tu ya watu wamatumia usafiri wa magari.
    .
    No.4: Seville, Hispania. Nao pia wamekuwa wakitegemea sana usafiri wa baiskeli kutokana na kuwepo barabara ambazo zinawapa uhuru kuenjoy usafiri huo.
    Bordeaux, FRANCE
    No.5: Bordeaux, Ufaransa, Barabara ambazo zimetengenezwa kwa ajili ya waendesha baiskeli ni kama km 200 katikati ya Mji. Hii imefanya kuwepo na ongezeko la watu wanaopendelea kutumia usafiri huo. Ufaransa ni moja ya nchi walio serious kabisa Ulaya kuhakikisha mazingira mazuri ya usafiri wa Baiskeli.
    Malmo CANADA
    No.6: Malmo, Sweden. Malmo ni mji wa tatu kwa ukubwa Sweden, wao mpaka zile barabara za baiskeli wamezipa majina, kama ilivyo kawaida kwa barabara kubwa magari. Waliamua hivyo iwe rahisi kwa mtu kuupata mtaa kwa kutumia GPS.
    Montreal CANADA
    No.7: Montreal, Canada. Barabara za mji wao ziko poa kabisa, japo ni mji mkubwa na uko busy lakini mazingira yanaruhusu hata kwa mwendeshaji wa baiskeli kuwa salama kabisa.
    Tokyo JAPAN
    No.8: Tokyo, Japan. Huu ni mmoja ya miji mikubwa duniani, wao wameweka utaratibu wa njia za baiskeli kutumiwa na wapita njia pia. Japo mfumo wa usafiri wa gari na treni za abiria uko vizuri kuuzunguka mji lakini watu wengi hupendelea pia baiskeli.
    Brazil Bicycle
    No.9: Rio de Janeiro, Brazil. Kwenye mafanikio waliyonayo wamefikia hatua ya kuweka mfumo wa baiskeli za kuazimisha, yani mtu anaichukua akimaliza mizunguko yake anairudisha na halipii gharama yoyote.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: Hii ndio miji 9 salama zaidi kuendesha baiskeli duniani.. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top