Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikatisha
kwenye migomba alipokuwa akikagua mifereji ya inayotiririsha maji
kuelekea kwenye mashamba ya ndizi akiongozana na Mh. Agrey Mwanri.
Akielezea
utekelezaji wa ilani ya uchaguzi katika jimbo hilo Mh. Agrey Mwanri
amesema ilani ya CCM imetekelezwa kwa kiwango kikubwa ambapo vijiji
vyote katika jimbo hilo vina maji safi na salama ya kunywa, Umeme
umefika katika vijiji vyote kinachondelelea ni usambazaji kwa kila
mwananchi, Suala la huduma za afya nalo liko vizuri kwani vimejenga
vituo vya afya karibu kila maeneo na baadhi ya zahanati zinamaliziwa
kujengwa.
Suala
la Elimu wakati mbunge huyo akiinga madarakani Siha kulikuwa na
sekondari moja, lakini sasa kuna sekondari 17 na ufaulu wa wanafunzi
umeongezeka kwa kiwangi cha juu, Maabara zinakamilishwa ambapo mabati
yamesambazwa karibu kila shule ili kukamilisha ujenzi wa maabara hizo.
Akizungumza
katika mkutano huo pamoja na mambo mengine Katibu Mkuu wa CCM amemsifu
Mh. Agrey Mwanri kwa kazi aliyoifanya katika jimbo hilo kwa kufanya kazi
vizuri na kuwaletea wananchi maendeleo na kuwaambia wananchi katika
mkutano huo kwamba kama kiongozi anafanya kazi nzuri hakuna haja ya
kubadilisha viongozi kama mashati, Mwacheni awaleteeni maendeleo.
Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Nape nnauye Katubu wa NEC Itikadi na Uenezi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoka kwenye chumba cha maabara cha hospitali ya wilaya Siha mara baada ya kuyakagua magari matatu ya kubebea wagonjwa.
Sehemu
ya jengo la hospitali hiyo ya wilaya ya Siha kama lionekanavyo
pichani,ambapo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alikwenda kukagua.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata
maelezo ya bwawa la umwagiliaji la Kishisha kata ya Ivaeny kutoka kwa
mbunge wa jimbo hilo Mh. Agrey Mwanri wakati alipokagua bwawa hilo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akichukua ndizi
wakati alipowatembelea akina mama wajasiriamali kabla ya kuhutubia
mkutano wa hadhara katika uwanja wa CCM wa wilaya ya Siha.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata
maelezo kutoka kwa akina mama wajasiamali wakimasai wanaojishughulisha
na kutengeneza bidhaa za urembo kwenye mkutano wa hadhara uwanja wa CCM
Siha.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuzindua ofisi ya CCM wilaya ya Siha, kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo Ndugu Oscar Temu.
Ndugu Kinana akitoka nje ya ofisi hiyo mara baada ya kuweka jiwe la msingi na kuikagua.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda mti wa kumbukumbu nje ya ofisi ya wilaya ya CCM Siha.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia
wananchi huku mvua ikinyesha hata hivyo wananchi hao waliamua kujikinga
na viti walivyokuwa wamevikalia ili wamsikilize Ndugu Kinana.





















