
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi kwa kupeleka
zege kwenye eneo husika wakati wa ujenzi wa daraja la Kisongo,ambalo
lilikuwa kero kubwa kwa wananchi kutokana na barabara ya eneo hilo
kulika na mmomonyoko wa udongo.
Ujenzi wa daraja la Kisongo ukiendelea kwa kasi,ambapo pia Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alikagua na kushiriki ujenzi wake.
Baadhi ya wananchi wa Kisongo wakipita juu ya barabara ambayo imeanza kuathirika na mmomonyoko wa udongo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuweka zege
wakati wa ujenzi wa kituo cha afya cha Manyire,ujenzi wa kituo hicho
unatarajia kuisha mwaka huu ambapo kiasi cha fedha zaidi ya shilingi
milioni 500 zitakuwa zimetumika kukamilisha ujenzi huo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Mjumbe wa
Halmashauri Kuu CCM Taifa kutoka wilaya ya Arumeru Magharibi Ndugu
Mathias Manga wakati wakiwasili kata ya Mlangarini tayari kushiriki
ujenzi wa Kituo cha Afya cha kijiji cha Manyire.
Shule ya Sekondari Sokoni II kama ionekanavyo pichani,ikiendelea
kujengwa vyumba 12 vya madarasa kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo
ambayo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alishiriki ujenzi
wake na kuzungumza na baadhi ya wazazu (hawapo pichani).Ujenzi wa vyumba
hivyo mpaka vitakapokamilika vinatarajia kugharimu kiasi cha fedha
zaidi ya shilingi milioni mia tisa
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi
Ngaramtoni ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa CCM ya sasa haitofanya
makosa, na kuwahakikishia kila atakayefanya makosa itabidi aubebe
msalaba wake.
Moja ya shina la wakereketwa
la Mateves lililofunguliwa na Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
Mbunge wa jimbo la Arumeru Magharibi Ndugu Goodluck Ole Medeye
akizungumza na wananchi wa
Kijiji cha Nduruma ambao walikuwa na malalamiko juu ya mradi wa maji wa
Nduruma kuonekana kupelekwa mashambani badala ya maeneo wanayoishi
wananchi.Ndugu Kinana wa pili kushoto alikuwepo kusikiliza malalamiko
hayo na kuwapatia majibu.
Mmoja
wa Wananchi akitoa malalamiko kuhusiana na mradi wa maji wa kijiji cha
Nduruma mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana (hayupo pichani).
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara
uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Ngaramtoni ambapo alitoa
sababu mbali mbali za dalili za kufa kwa upinzani nchini.
Mbunge wa jimbo la Arumeru Magharibi Ndugu Goodluck Ole Medeye akihutubia wananchi waliojitokeza kwa
wingi kwenye viwanja vya shule ya msingi Ngaramtoni,Arusha.












