LISTI YA SIMBA VS MGAMBO...
Kuna
mambo mengi yanahitajika kubadilishwa katika soka la Tanzania. Huenda
mengine yanaweza kuwa ya kipuuzi kabisa na hautegemei kuona yanaendelea
lakini hakuna anayeyafanyia kazi.
LISTI YA BARCELONA VS MAN CITY....
Kwanini
hawajayafanyii kazi? Jibu hawajali, hawaupendi mpira na wanachoangalia
wao ni kuingiza fedha kutoka katika mpira. Huu ni upuuzi.
Unapokuwa jijini Dar es Salaam, mechi za Ligi Kuu Bara zimekuwa zikiandaliwa kwa mpangilio mzuri sana.
Kitu kidogo nitakupa mfano, karatasi ya listi ya wachezaji. Utaona imepangiliwa vizuri kabisa tena kwa kuchapishwa.
Lakini
mechi nyingi za mkoani, karatasi zinachukuliwa zile za daftari au listi
inaandikwa hovyohovyo tu. Hauwezi ukasema hii ni hadhi ya Ligi Kuu Bara.
Karatasi
ya listi za wachezaji ya Ligi Kuu Bara, mechi kati ya Simba dhidi ya
Mgambo haina tofauti na mechi ya mchangani. Upuuzi.
Chama cha
Soka Tanzania, kinapata mgawo katika mapato ya mechi hiyo. Kununua
karatasi na kufanya mambo kwa mpangilio haiwezekani?
Hakuna kiongozi anayeona hilo si sahihi, hawana aibu na wanakubali vipi ifanyike?
Kama hao
wanakubali, vipi uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) nao
unakubali hali hiyo? Unaona sawa kwa kuwa mambo yanakwenda?
TFF inapaswa kuwa kiongozi anayeangalia uhakika na hadhi ya inachokiongoza. Mabadiliko yafanyike. Ala!

