Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa barabara ya
Mwanama- Olorien ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami,Ndugu Kinana pia
aliitembelea na kuikagua barabara hiyo.
Ujenzi
wa barabara ya Mwanama- Olorien ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami
ukindelea ambapo Ndugu Kinana pia aliitembelea na kuikagua.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akitembelea kiwanda cha
General Tyre eneo la Themi,jijini Arusha,ambapo Kiwanda hicho Serikali
imeamua kukifufua na kuanza kuzalisha upya bidhaa zake kupitia shirika
la Maendeleo la Taifa (NDC),pichani kati ni Kaimu Mkuregunzi wa
NDC,Bwa.Mlingi Mkucha na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha,Onesmo Ole
Nangolo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akisikiliza malalamiko ya
baadhi ya waliokuwa wafanyakazi wa kiwanda cha shirika la General
Tyre,ambao Ndugu Kinana ameahidi kuyafanyia kazi na kuhakikisha
wafanyakazi hao wanapata haki yao.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa ameambatana na Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye sambamba na viongozi wengine wa
chama hicho wakitembelea kiwanda cha nguo cha Kiltex,ambapo kimefungwa
na kusimamisha uendeshaji wake,ambapo kwa miaka mitatu kiwanda hicho
kiligeuzwa kuwa ghala la kuhifadhia nafaka,hku mitambo yake yote ikiwa
imeondolewa na kupelekwa kusikojulikana,
Mlinzi
Mkuu wa Kiwanda cha Kiltex,Mathias Mahundi akifafanua jambo kwa Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana,na kulia ni Mkuu mpya wa Wilaya ya
Arumeru na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh.Asnah Mwilima.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizunguza na Halmashauri kuu ya
CCM Wilaya,mapema leo jijin Arusha,ambapo pia alipokea taarifa za kazi
ya chama na serikali.








