Mkuu
wa Mkoa wa Mtwara,Mh. Halima Dendegu akifungua rasmi semina maalum kwa
Maafisa Utumishi kutoka Mikoa ya Lindi la Mtwara Juu ya Maendeleo ya
Mfuko wa Pensheni wa GEPF,uliofanyika Mkoani Mtwara.Katika hotuba yake
ya Ufunguzi,Mh. Dendegu ameupongeza na kuushukuru uongozi wa Mfuko wa
GEPF kwa kuifikisha elimu hiyo katika mikoa hiyo ya kusini.
Meneja
Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa GEPF,Bw. Aloyce Ntukamazina akiwasilisha
mada juu ya maendeleo ya Mfuko wa GEPF, mafao mapya yatolewayo pamoja
na faida za kuwa mwanachama,wakati wa semina maalum kwa Maafisa Utumishi
kutoka Mikoa ya Lindi la Mtwara.
Afisa
Utumishi kutoka wilaya ya Kilwa,Bw. Masimba akitoa neno la shukrani kwa
niaba ya washiriki wenzake mara baada ya kumalizika kwa semina hiyo
maalum.
Mmoja wa Washiriki wa Semina hiyo akitoa ushauri kwa uongozi wa Mfuko wa GEPF mbele ya Mkuu wa Mkoa.
Meneja
wa Mfuko wa Pensheni wa GEPF Mkoa wa Mtwara,Bw. Deogratias Kakoko
aliyeketi kushoto kwa Mkuu wa Mkoa wakisikiliza kwa makini ushauri
uliotolewa na washiriki wa semina hiyo.

