WAZIRI
wa Maliasili na Utalii Lazaro, Nyalandu leo amepokea ndege aina ya
Micro Light Nyinja 5H-HEL, kutoka kwa kampuni inayojihusisha na masuala
ya utalii ya Tanganyika Wildlife Safari itakayosaidia harakati za
kukomesha masuala ya uuaji wanyama pori na ujangili.
Akipokea
ndege hiyo jijini Dar es Salaam,Waziri Nyalandu alisema ndege hiyo ni
mpya kabisa na ya usalama wa hali ya juu kutokana na muunekano wake kuwa
wakisasa zaidi.
"Hii
ndege ni salama zaidi kwasababu yenyewe imejengwa na parachuti yake
endapo kunatokea chochote wakati ikiwa angani inafunguwa parachuti
ambayo itaisaidia yenyewe pamoja na watu waliomo hivyo ni ya uhakika
zaidi". alisema Nyalandu.
Nae
Mwenyekiti wa kampuni iliyotoa ndege hiyo ya Tanganyika Wildlife Safari,
Eric Pasanisi, alisema ndege hiyo inathamani ya Dola laki mbili na
ishirini elfu ($220,000), na kueleza sifa mbalimbali za ndege hiyo.
"Ndege
hii ni ndege yenye spidi ndogo zaidi kuliko ndege yeyote, kwani mwendo
wa ndege hii ni karibu sawa na mwendo wa gari tu, kutokana na hali hiyo
itakuwa rahisi zaidi kuwabaini majangili walipo kwavili mwendo wake ni
mdogo." alifafanua Eric.
Aidha Eric alisema mbali na hilo ndege hiyo pia inatumia petroli hivyo ni ya gharama nafuu zaidi kuliko ndege za kawaida.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Lazari Nyalandu (kushoto) akikabidhiwa ndege
aina ya Micro Light Nyinja, 5H-HEL, na Mwenyekiti wa Kampuni ya Utalii
ya Tanganyika Wildlife Safari, Eric Pasanisi, werngine ni Askari wa
kikosi cha wanyamapori walio hudhuria makabidhiano hayo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akiwa na Rubani wa ndege aina ya
Micro Light Nyinja, muda mfupi kabla ya kukabidhiwa ndege hiyo. Ndege
hiyo ambayo imenunuliwa na kampuni ya Tanganyika Wildlife Safari
ilikabidhwa kwa Waziri Nyalandu kwaajili ya kufuatilia majangili kwenye
hifadhi za taifa.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Lazari Nyalandu akizungumza jambo mara baada ya
kukabidhiwa ndege aina ya Micro Light Nyinja, 5H-HEL, na Mwenyekiti wa
Kampuni ya Utalii ya Tanganyika Wildlife Safari, Eric Pasanisi (kulia),
werngine ni Askari wa kikosi cha wanyamapori walio hudhuria makabidhiano
hayo.

