Afisa
Mwendeshaji Mkuu wa UTT AMIS Bw.Simon Migangala akiongea na waandishi
wa habari jana Dar es salaam kuhusiana na ufanisi wa mifuko kwa kipindi
cha miezi sita iliyopita.
UTT
AMIS ndiyo waendeshaji na waanzilishi wa mifuko ya uwekezaji wa pamoja
nchini.Mpaka sasa wanaendesha mifuko mitano ya uwekezaji ambayo ni Mfuko
wa Umoja, Mfuko wa wekeza Maisha,Mfuko wa Watoto, Mfuko wa Kujikimu na
Mfuko wa Ukwasi yenye zaidi ya shilingi bilioni 227.
Bwana
Migangala aliwaambia waandishi wa habari kuwa kwa ujumla ukuaji wa
mifuko umekua mzuri na umewezasha kutoa faida nzuri kwa wawekezaji wake
zaidi ya 100,000 kwa kipindi cha miezi sita iliyopita.
Mfuko
uliotoa faida nzuri zaidi ni Mfuko wa Watoto ambao ulitoa asilimia
51.19 ukifuatiwa na Wekeza Maisha uliotoa asilimia 45.23
Mfuko wa tatu ni Umoja ambao ulikua kwa asilimia 38.46, wanne Kujikimu alikua kwa asilimia 36.77 na Ukwasi kwa asilimia 11.46
Alisema
kimsingi wanafurahia na wanajivunia faida hiyo waliyopata wawekezaji
wao.Ukuaji huu umechangiwa na ufanisi mzuri wa soko la Hisa la Dar es
salaam , masoko ya fedha ambako mifuko pia huwekeza na weledi wa meneja
wa Mifuko (UTT AMIS) katika kuwekeza na kusimamia mifuko.
Katika kipindi hicho cha miezi sita thamani halisi za vipande vya mifuko viliongezeka kama ifuatavyo;
Kipande
cha Mfuko wa Umoja kiliongezeka kutoka shilingi 365.6892 hadi shilingi
435.9008,Wekeza Maisha kilitoka shilingi 237.5386 hadi 291.1558 kwa
Mfuko wa Watoto kiliongezeka kutoka shilingi 213.72 hadi shilingi
268.3172
Mfuko
wa Kujikimu kutoka shilingi 118.1779 hadi shilingi 131.1440(ukijumuisha
na gawio la shilingi 4 kila baada ya miezi mitatu) na mwisho Mfuko wa
Ukwasi toka shilingi 114.3608 hadi shilingi 120.9362.
Ongezeko
hilo linathibitisha ukuaji wa mifuko yetu na tunawahamasisha watanzania
wajiunge katika mifuko hii waweze kuwekeza fedha zao na kupata faida
maridhawa.Tunaendelea kuwaambia kuwa ni fedha zako,ni akiba yako,ni
uwekezaji wako, faida ni yako! UTT AMIS tunawezesha! Hakika
tutaendelea kuwa ‘Mshirika hakika katika uwekezaji’


