Wafungwa
wa Gereza Kuu Ukonga, Jijini Dar es Salaam wakiendelea na ushonaji wa
nguo za aina mbalimbali kama wanavyoonekana katika picha. Jeshi la
Magereza nchini linatekeleza ipasavyo jukumu lake la Urekebishaji kwa
kuwapatia ujuzi wa fani mbalimbali Wafungwa wanapokuwa wakitumikia
vifungo vyao Magerezani.
Wafungwa
wa Gereza Kuu Ukonga, Jijini Dar es Salaam wakikata vitambaa vya nguo
kabla ya kuanza kushona nguo za Wafungwa Magerezani. Wafungwa hao
hujifunza Stadi mbalimbali za ujuzi ambazo huwasaidia kujipatia kipato
mara tu wanapomaliza kifungo chao.
Aina
za nguo mbalimbali ambazo tayari zimeshonwa kwa Ustadi Mkubwa na
Wafungwa wa Gereza Kuu Ukonga Dar es Salaam. Gereza Kuu Ukonga Dar es
Salaam limejizolea umaarufu mkubwa hapa nchini kwa kutekeleza ipasavyo
Programu mbalimbali za Urekebishaji wa Wafungwa kwa Vitendo

Mkuu
wa Kiwanda cha Gereza Kuu Ukonga, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Ismail
Mlawa akiongea na Wanahabari(hawapo pichani).Picha zote na Lucas Mboje
wa Jeshi la Magereza

