Milionea
kupitia Promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom
Tanzania,Ibrahim Ibrahim (kushoto) akimkabidhi hundi yenye thamani ya
shilingi Milioni 10/- Zuwena Rajabu(kulia)aliyeibuka mshindi wa kitita
hicho kupitia Promosheni hiyo wiki hii.Anayeshuhudia katikati ni Meneja
Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu.Hafla hiyo ilifanyika Tabata
Segerea jijini Dar es Salaam,Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa
kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.
Mshindi
wa Promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,Zuwena
Rajabu(kulia)akisoma hundi yake yenye thamani ya shilingi Milioni 10/-
wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa hundi hiyo na Milionea mwenzake
Ibrahim M. Ibrahim(kushoto)na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Matina
Nkurlu(katikati).Hafla hiyo ilifanyika Tabata Segerea jijini Dar es
Salaam.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO
kwenda namba 15544.
Milionea
kupitia Promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom
Tanzania,Ibrahim Ibrahim (kushoto) na Meneja wa kampuni hiyo Matina
Nkurlu(katikati)wakimpongeza Mshindi wa Promosheni ya
Jaymillions,Zuwena Rajabu baada ya kumkabidhi hundi yake yenye thamani
ya kitita cha shilingi Milioni 10/-alizojishindia kupitia promosheni
hiyo.Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika Tabata Segerea jijini Dar es
Salaam.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO
kwenda namba 15544.
Zuwena
Rajabu ambaye ni Mshindi kupitia Promosheni ya Jaymillions
inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,akiongea na waandishi wa habari baada
ya kukabidhiwa hundi yake yenye thamani ya shilingi Milioni 10/- wakati
wa hafla fupi iliyofanyika Tabata Segerea jijini Dar es Salaam ya
kukabidhiwa hundi hiyo na Milionea mwenzake Ibrahim M. Ibrahim na Meneja
Uhusiano wa kampuni hiyo Matina Nkurlu(hawapo pichani).Ili mteja kujua
kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.
Meneja
Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(katikati)akimsomea hundi
yake Zuwena Rajabu(kulia)wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi hundi hiyo
yenye thamani ya kitita cha shilingi milioni 10/- alizojishindia kupitia
promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na kampuni hiyo hivi
karibuni.Anayeshuhudia kushoto ni Milionea kupitia Promosheni hiyo
Ibrahim M. Ibrahim.Hafla hiyo ilifanyika Tabata Segerea jijini Dar es
Salaam. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO
kwenda namba 15544.
Binti
msusi anayefanya kazi ya ususi na mkazi wa Tabata Segerea Zuwena Rajabu
(22) leo amekabidhiwa kitita cha shilingi milioni 10/-alizojishindia
kupitia promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa ka Vodacom Tanzania.
Zuwena
alikabidhiwa fedha zake na milionea mwenzake aliyemtangulia Ibrahim M.
Ibrahim,Ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha St.Joseph yeye
alikabidhiwa kitita chake cha milioni 10 wiki iliyopita.Makabidhiaano
hayo yalifanyika katika saluni anapofanyia kazi Zuwena iliyopo Tabata
Segerea mbele ya wafanyakazi wenzake na waandishi wa habari.
Akiongea
muda mfupi baada ya kupokea fedha zake za ushindi,Zuwena alisema
anamshukuru Mwenyezi Mungu amemuona na ameweza kusikia maombi yake ya
kupata mtaji wa kuanzisha saluni yake ya kike ya kisasa na duka la kuuza
Vipodozi imetimia.
“Naishukuru
sana Vodacom Tanzania wamefanya ndoto yangu ya kuwa mfanyabiashara
mkubwa kutimia na huu ni uthibitisho kuwa promosheni ya Jaymillions
imelenga kuwakomboa wanyonge kutoka hali ya chini na kuwapandisha kwenda
hali ya juu”.Alisema Zuwena kwa furaha .
Promosheni
ya Jaymillions iliyoanza katikati ya mwei Januari mwaka huu ambayo
itadumu kwa muda wa siku 100 imeleta faraja na itaendelea kuleta faraja
na mafanikio kwa wateja wa kampuni hiyo kwa kuweza kujinasua katika hali
duni ya maisha na maisha kuwa murua na hadi kufikia sasa
amekwishapatikana mshindi mmoja wa milioni 100/-,washindi wanne wa
milioni 10/-na washindi 38 wa milioni 1/-.
Mshindi
wa milioni 100/-ni Uwezo Madengenya kutoka wilayani Kilolo mkoani
Iringa.Washindi wa milioni 10/-mbali na Zuena aliyekabidhiwa kitita
chake leo ni Hyness Petro Kanumba kutoka Rukwa,James Mangu (Mwanza), na
Deborah Stanley ambaye naye ni anafanya kazi ya ususi na mkazi wa
Kimara kwa Komba jijini Dar es Salaam.
Meneja
Uhusiano wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu,akiongea katika hafla hiyo
alimpongeza mshindi huyo na kusema kwamba fedha hizo zimeenda kwa
mshindi sahihi kwani mshindi huyu ana malengo mazuri ya matumizi ya
fedha zake kwa kujiendeleza kibiashara.
Pia
aliwahimiza wateja wote kuchangamkia promosheni ya Jaymillions katika
kipindi hiki ambacho inakaribia kufika mwishoni ili wajishindie kwa
kuhakikisha wanatuma neno JAY kwenda namba 15544 ili kutopoteza bahati
zao za kushinda.Aliitaja njia nyingine ya kushinda kuwa ni kutuma neno
AUTO kwenda namba 15544 iwapo simu haina fedha ambapo mteja akiweka
fedha anakatwa shilingi 300/-tu.






