https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    Nigeria Yafanya Mageuzi...Mgombea wa Upinzani Aibuka Mshindi wa Kiti Cha Urais


    Mgombea wa upinzani nchini Nigeria Muhammadu Buhari ameibuka mshindi wa kiti cha urais dhidi ya Rais Goodluck Jonathan katika uchaguzi uliofanyika Jumapili nchini humo.

    Kwa mujibu wa Reuters, Buhari wa chama cha upinzani cha APC amepata kura million 15.4 dhidi ya kura million 13.3 alizopata Jonathan.

    Chama cha Rais Jonathan All Progressives Congress (APC) kimesema kuwa Jonathan amekubali matokeo na amempigia simu Buhari kumpongeza kwa ushindi huo.

    Ushindi huu wa Buhari ambaye ni kiongozi wa zamani wa jeshi unaandika historia katika taifa hilo kwa kuwa ni mara ya Kwanza kwa chama cha upinzani kushinda kiti cha urais kwa njia ya kidemokrasia

    Baadhi ya waangalizi wa uchaguzi huo wamepongeza namna uchaguzi ulivyoendeshwa licha ya kuripotiwa kwa hujuma katika baadhi ya maeneo ambazo zilisababisha hofu ya kutokea kwa vurugu.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: Nigeria Yafanya Mageuzi...Mgombea wa Upinzani Aibuka Mshindi wa Kiti Cha Urais Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top