Dkt.Jakaya
Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya jijini
Windhoek Namibia ambapo walihudhuria sherehe za kuapishwa Rais mpya wa
Namibia.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na marais wastaafu Ali Hassan
Mwinyi(kulia) na Benjamin William Mkapa(kushoto) katika uwanja wa ndege
wa kimataifa wa Hosea Kutako jijini Windhoek Namibia leo.Viongozi hao
walihudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 25 ya Uhuru wa Namibia
ambapo pia Rais wa awamu ya tatu wa Namibia Dkt.Hage Geingob aliapishwa
katika uwanja wa Independence jijini Windhoek.Chama cha ukombozi cha
Namibia SWAPO kilizaliwa nchini Tanzania na kuendesha harakati za
ukombozi mpaka mwaka 1990 ambapo nchi hiyo ilipata uhuru.
(picha na Freddy Maro).
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake akikutana na Rais Uhuru
Kenyatta wa Kenya katika Hoteli ya Safari Court jijini Windhoek N amibia
jana

