https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    Rais Kikwete Awasili Marekani Kwa Mwaliko wa Umoja Wa Mataifa


    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Jumapili, Machi 29, 2015 amewasili jijini New York, Marekani kwa mwaliko wa Umoja wa Mataifa.
     
    Miongoni mwa mambo mengine, Rais Kikwete amefunguia rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa, na Jumatatu Machi 30, 2015 amealikwa kuhutubia Baraza la Umoja wa Mataifa la Uchumi na Jamii (ECOSOC - UN).
    Rais Kikwete akilakiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatifa Dkt Mahadhi Juma Maalim alipowasili jijini New York, Marekani. 
    Rais Kikwete akisalimiana na Waziri wa WAZIRI wa Kazi na Ajira, Mhe. Gaudensia Kabaka anayefuatiwa na Waziri wa Fedha wa Zanzibar Mhe. Omar Yussuf Mzee ...
    Jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
    Rais Kikwete akikata utepe kufungua rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani

    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: Rais Kikwete Awasili Marekani Kwa Mwaliko wa Umoja Wa Mataifa Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top