Kumekuwa na mbinu mbalimbali ambazo wato wamekuwa wakibuni kila siku kusafirisha dawa ya kulevya, unaikumbuka ya Nigeria ambayo jamaa aliweka dawa hizo kwenye viatu vya kike? Zipo nyingine nyingi tu tumeshasikia.. Nakusogezea hii nyingine toka China.
Friday Ogbonna amekamatwa Uwanja wa Ndege Nigeria akiwa na mizigo yake tayari kwa safari kuekea China, amekutwa na dawa hizo zenye uzito wa kg 35 ambazo zilifichwa katikati ya sausage.
Kikosi cha National Drug Law Enforcement Agency walifanikiwa kumkamata Friday katika
uwanja wa ndege Lagos, mwenyewe anasema anajutia kosa hilo kwa kuwa
hakujua kama alichokuwa akisafirisha ni dawa, mtu aliyemuagiza aliahidi
kumlipa Naira 100,000 (sawa na laki 9 Tshs) baada ya kufikisha mzigo
China.

