Baadhi ya mashuhuda wakielekea eneo la tukio |
Mtu
mmoja aliyefahamika kwa jina la Shedrack Misago Ndironkeye(78) mkazi wa
kitongoji cha Mkagobero kijiji cha kabanga wilayani Ngara mkoani kagera
alikutwa ameuwawa kikatili kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na
baadhi ya sehemu za mwili wake kukatwa na kitu chenye ncha kali na watu
wasiojulikana kisha mwili wake kuutelekezwa kichakani huku kichwa kikiwa kimepondwa vibaya na kuwekewa kokoto.
Tukio
hilo lilitokea usiku wa kuamkia Alhamisi ya tarehe 26/03/2015, ambapo
inadaiwa marehemu alikumbwa na mauti hayo akitokea kilabuni kuelekea
nyumbani kwake majira ya usiku wa saa mbili nakuendelea. Kamanda wa
polisi kituo cha Kabanga OCS Benard Joseph alithibitisha kutokea kwa
tukio hilo ambapo jeshi la polisi linawasaka waliohusika na tukio hilo
maana mpaka sasa hakuna mtu anayeshikiliwa kwa kuhusika na mauaji hayo.
Mwili wa marehemu ukiwa umetelekezwa porini |