Matukio
mengi ya matumizi mabaya ya mtandao yamekuwa yakiripotiwa sana, iko
ishu ya watu kuzushiwa vifo, picha chafu kusambazwa mitandaoni..
Nimekutana na hii story imebidi niisogeze hapa huenda wewe hujaipata.
Wanafunzi wa Shule West Sussex Uingereza, inafanya uchunguzi ili kujua wanafunzi waliohack akaunti ya Twitter ya Shule hiyo.
Watu walivamia akaunti hiyo wakaanza kupost picha za Mkuu wa Shule akiwa mtupu.
Uchunguzi umeonesha kuwa picha hizo zilikuwa za kutengenezwa hazikuwa za ukweli.
Watu walioingia kwenye akaunti ya Shule hiyo walishangazwa kukuta picha za utupu za Mkuu wa shule hiyo.
Polisi wanafanya uchunguzi kujua namna
akaunti hiyo ilivyovamiwa wakati ni watu wachache wanaojua namba ya
siri, Shule hiyo imeomba radhi kutokana na tukio hilo kupitia akaunti
hiyo ya twitter na kusema uchunguzi unaendelea.