Wakwanza
kulia ni Meneja Masoko wa Airtel Tanzania Aneth Muga akiwa ameshilia
bango linaloonyesha huduma mpya ya Airtel Wi-Fi intaneti maalum kwa
wanavyuo iliyozinduliwa rasmi kwa mara ya kwanza Mwanza katika chuo cha
St Augustine (SAUT) pamoja nae anaefuata ni raisi wa serikali ya
wanafunzi Sogone Wambura, Mshauri wa wanafunzi chuoni hapo bw,Liberates
Ndegeulaya na Afisa masoko wa Airtel Mwanza Bw, Emanuel Raphael
Afisa
masoko wa Airtel bw, Prospa Mwanda akitoa maelekezo ya jinsi huduma mpya
ya Airtel Wi-Fi inavyofanyaka kazi kwa kasi kwa Raisi wa wanafunzi chuo
kikuu cha SAUT mwanza Bw, Sogone Wambura (wakwanza kulia) na Makamu wa
Raisi wa chuo hicho Bi, Pearl Mecar (kati) mara baada ya Airtel kuzindua
huduma hiyo chuoni hapo jana.
Meneja
Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga akionyesha kwa wanafunzi wa SAUT Mwanza
(hawapo pichani) muonekano wa vocha za huduma mpya ya Airtel Wi-Fi
intaneti iliyozinduliwa chuoni hapo jana maalumu kwaajili ya kuwapa
wanafunzi intaneti nafuu na yenye kasi zaidi.
Mshauri
wa wanafunzi chuo cha St. Augustine Mwanza (SAUT) akiongea na wanafunzi
(hawapo pichani) kuitumia vyema huduma iliyozinduliwa na Airtel ya
Wi-Fi intaneti ili kutimiza uhitaji wao katika masomo na kuongeza ufaulu
chuoni hapo. Hafla ya uzinduzi ilifanyika chuoni hapo jana.
Kampuni
ya simu za mkono ya Airtel Tanzania katika muendelezo wa kutoa huduma
bora na nafuu nchini imezindua huduma mpya ya kisasa ya UNI Wi-Fi
itakayowaweza wanafunzi vyuoni kufurahia huduma ya Intaneti yenye kasi
zaidi
Akiongea
wakati wa uzinduzi uliofanyika chuo kikuu cha SAUT Mwanza Meneja Mauzo
wa Kanda ya Ziwa Bw, Raphael Daudi alisema “huduma ya Airtel UNI Wi-Fi
tumeianzisha kwaajili ya kuwapatia wanafunzi huduma nafuu ya intaneti
yenye kasi zaidi wakati wanapofanya shughuli zao za masomo au
wanapoingia katika mitandao ya jamii kupata taarifa mbalimbali muhimu”
Ulimwenguni
Intaneti sio kitu cha anasa tena na pia kutokana na kasi ya uhitaji
wake kwenye mambo ya maendeleo ya uchumi na kijamii kwenye makundi
tofauti vikiwemo vyuo vya elimu ya juu Airtel tumeona ni vyema kuja na
ubunifu huu kuleta suluhisho kwenye kuwahudumia wateja wetu”
Leo
huduma ya intaneti kupitia Airtel UNI Wi-Fi hapa Chuo cha St, Augustine
Mwanza (SAUT) ni rahisi na nafuu kabisa kupitia Airtel
Kwa
Upande wake Meneja Masoko wa Huduma hiyo Bi, Aneth Muga amesema “Airtel
Uni Wi-Fi tunayozindua leo nimuendelezo wa mikakati yetu ya Airtel kutoa
huduma nafuu kwa wanafunzi, mwishoni mwa mwaka jana pia tulizindua Uni
255 vocha kwenye vyuo mbalimbali ili kuwapatia huduma ya bando za
Intaneti, SMS pamoja na muda wa maongezi nafuu zaidi kuliko zote”
Leo hii Wi-Fi vocha ipo ya Siku, Wiki, Mwezi au bando la usiku kwa gharama nafuu ya hadi shilingi mia tano kwa GB 1 kwa siku.
Unachotakiwa
kuwa nacho ili kufaidi huduma hii ni kuwa na kifaa chochote kinachoweza
kutumia Wi-Fi kama vile smartphone, laptop, tablet, Camera, printer na
utaunganishwa bila kujali unatumia laini ya Airtel au mtandao wowote.
“Leo
tumeanzia hapa SAUT lakini tutahakikisha inasambaa vyuoni kote na baadae
nchi nzima ili vijana na wale wote wanaokwenda na wakati waweze
kufaidika nayo katika matumizi ya kimtandao” alimaliza kusema Bi Muga
Kwa
upande wake mgeni rasmi katika uzinduzi huo mkuu wa Chuo hicho Bw,
Liberatus Ndegeulaya alisema “hapa chuoni SAUT tumefarijika sana kuona
Airtel mara zote mnaanzia kwetu mnapotaka kuzindua huduma hizi rafiki
kwa mawasiliano. Kwa elimu ya sasa hii Wi-FI ni muhimu sana inarahishia
wanafunzi wetu na hata sisi walimu katika ufundishaji”
Natoa wito kwa wanafunzi wote kuitumia Airtel Wi- Fi kama nyenzo ya kufikia mmalengo ya elimu yao
Nae
Raisi wa serikali ya wanafunzi Sogone Wambura aliishukuru Airtel huku
akiitikia wito wa kuitumia huduma hiyo kwa manufaa ya kupandisha kiwango
cha elimu nchini sambasamba na ukuaji wa teknolojia mbalimbali.
“Asanteni
Airtel kwa ubunifu huu na kuleta Airte Wi-Fi sisi wanafunzi
tutahakikisha tunajiwekea utaratibu wa kuitumia katika utaratibu unaofaa
na wenye manufaa ya kwa elimu nan chi yetu’ alisema Wambura Raisi wa
wanafunzi SAUT.