MAUJAJI
17 wa dhehebu la Kihindu kutoka India wamepoteza maisha leo katika ajali
ya basi walilokuwa wakisafiria katika Wilaya ya Dhading karibu na Mji
wa Kathmandu nchini Nepal.
Katika
ajali hiyo, maujaji 27 wamejeruhiwa huku watano kati yao wakiripotiwa
kuwa katika hali mbaya, Ubalozi wa India nchini Nepal umeeleza.
Basi hilo
lilikuwa likitoka Kathmandu kwenda Mji wa Gorakhpur. Maujaji hao
walikuwa wakirejea nyumbani baada ya kumaliza kuhiji katika Hekalu la
Pashupatinath mjini Kathmandu.
Kupitia
mtandao wa Twitter, Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi ametuma salamu
za rambirambi kwa ndugu na jamaa waliopoteza maisha katika ajali hiyo
huku akieleza kuwa watu wao waliopo katika ubalozi wa India nchini Nepal
wamefika eneo la tukio mapema na kwa sasa wapo katika kila hospitali
walipopelekwa majeruhi wa ajali hiyo na wanatoa huduma zinazostahili.
Kutokana
na taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Basudev Ghimire ni kwamba
basi hilo lilipoteza mwelekeo na kupinduka kisha kudondoka chini umbali
wa mita 150 kutoka barabarani.