MAGARI
mawili yanayosafirisha abiria jijini Dar es Salaam, leo yamegongana
katika ajali iliyotokea eneo la Mkwajuni na kujeruhi vibaya abiria wake.
Mashuhuda
wa tukio hilo wamesema ajali hiyo imesababishwa na gari lililokuwa
linatokea Kawe kuelekea Kariakoo lililokuwa linafuka moshi na
kusababisha njia nzima kujaa moshi na hivyo kusababisha magari hayo
kugongana na kuangukia bondeni.
Chanzo
kutoka eneo la ajali kimesema majeruhi wengi wamepelekwa hospitali ya
Mwananyamala na Muhimbili ambapo hali zao zilikuwa hazijulikani wakati
mtandano huu unaingia mtamboni.