Aliyekuwa
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Kata ya Makuyuni, Badi Mandali akizungumza
mara baada ya kukabidhiwa kadi ya uanachama wa Tanzania Labour Party
(TLP) katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Kata ya
Makuyuni, Himo mkoani Kilimanjaro, juzi. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa
chama hicho, Augustine Mrema na mkewe Rose Mrema.
Mbunge
wa Vunjo, Augustine Mrema akiwa na wanachama wapya wa chama hicho
waliotoka NCCR-Mageuzi, CCM na Chadema mara bada ya kuwakabidhi kadi
mpya mara baada ya mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya
Kata ya Makuyuni, Himo mkoani Kilimanjaro, juzi.
Aliyekuwa
Diwani wa Kata Mwika Kusini (TLP), kabla ya kutimuliwa kwa madai ya
kukisaliti chama hicho Meja Jesse Makundi akizungumza kuhusiana na
tuhuma zinazomkabili wakati wa mkutano wa hadhara katika Kijiji cha
Lole, jimboni Vunjo mkoani Kilimanjaro juzi.Mbunge
wa Vunjo (TLP), Augustine Mrema akiongoza maandamano ya wakazi wa
Kijiji cha Lole, Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro mara baada ya
kumaliza mkutano wa hadhara ikiwa ni sghemeu ya ziara yake jimboni humo
juzi.
Mbunge
wa Vunjo (TLP), Augustine Mrema akiongoza maandamano ya wakazi wa
Kijiji cha Lole, Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro mara baada ya
kumaliza mkutano wa hadhara ikiwa ni sghemeu ya ziara yake jimboni humo
juzi.
Wanafunzi
wa shiule ya sekondari Muungano wakimpokea Mbunge wa Vunjo, Augustine
Mrema mara baada ya kuwasili shuleni hapo, Himo Mkoani Kilimanjaro,
juzi.
Mbunge
wa Vunjo, Augustine Mrema akishiriki katika ujenzi wa bweni la
wanafunzi katika Shule ya Wasichana Wenye Vipaji Maalum ya Muungano,
Himo Mkoani Kilimanjaro, juzi.
Jengo la shule
……………………………………………………………….
Mwandishi Wetu,
Mbunge
wa Vunjo, Augustine Mrema ametangaza mkakati wa kuisambaratisha
NCCR-Mageuzi Vunjo kwa kuzindua rasmi kampeni inayoitwa ‘TOKOMEZA MBATIA
VUNJO’.
Akizungumza
wakati wa mkutano na wanachama wa chama hicho katika Kata ya Makuyuni
Himo, kitongoji cha Kiriche, juzi, Mrema alisema operesheni hiyo ina
lengo la kuhakikisha jitihada za Mbatia kulitwaa Jimbo hilo
hazifanikiwi.
Mrema
ambaye alisema operesheni hiyo ni majibu kwa Mbatia ya kauli yake
ambaye alitangaza ‘Delete TLP/ Mrema’, alisema mwanasiasa mwenzake huyo
anatumia propaganda chafu dhidi yake ikiwa ni pamoja na kudai kazeeka,
hafai na hana uwezo wa kuwaongoza Vunjo.
“Mimi
kuanza sasa natangaza ‘TOKOMEZA MBATIA VUNJO’ na ninasema nipo fiti,
hafi mtu hapa na nina uwezo ninao wa kuendelea kuwaongoza Vunjo kwani
nina mtaji wa kutosha wa watu” alisema.
Mrema
aliitangaza operesheni hiyo muda mfupi baada ya kuwakabidhi kadi
viongozi sita wa NCCR Mageuzi wa Kitongoji cha Kiriche akiwemo
Mwenyekiti wa chama hicho Kata ya Makuyuni, Badi Mandari na wengine 50
kutoka vyama tofauti.
Mbunge
huyo alisema kuwa wakati wa kujua mbivu na mbichi ni sasa na kubainisha
kuwa kuna wanachama wa TLP ambao walirubuniwa na Mbatia lakini baada ya
kuujua ukweli wamerudi katika chama chake.
Mrema
ambaye pia alimkabidhi makalavati manne kwa ajili ya ujenzi wa daraja
katika kitongoji cha Kiriche, alisema mfuko wa Jimbo hadi sasa umetumia
jumla ya shilingi milioni 15.1 kwa ajili ya shughuli za maendeleo katika
Kata hiyo.
Mara
baada ya kupokea makalavati hayo, Mandari, alisema wananchi wa eneo
hilo vipindi vya mvua wamekuwa wakipata adha kubwa ambayo wakati
mwingine imekuwa ikiwafanya wakakosa mawasiliano ya barabara na wenzao
wa maeneo vijiji vingine.
Katika
hatua nyingine, Mrema alikataa kuwasamehe mbele ya mkutano huo madiwani
wawili waliofukuzwa katika chama hicho, Yolanda Lyimo wa Kata ya Kilema
Kati na Meja Jesse Makundi wa Mwika Kaskazini.
“Nimesikia
maombi yenu ya msamaha, lakini katika chama sikuwafukuza mimi Mrema,
bali ni vikao vya chama hivyo suala lenu nalipeleka mbele ya Kamati Kuu
lakini akawashauri ili Kamati Kuu iweze kusikiliza maombi yao sharti
muondoe kesi mnayodai fidia dhidi yangu na Naibu Katibu Mkuu, Nancy
Mrikaria ya shillingi millioni 500” alisema Mrema.