
Katika
jitihada za kupambana na uhalifu wa kimtandao ili kuhakikisha
upatikanaji wa huduma za kibenki katika mazingira salama zaidi, Benki ya
Exim imetoa wito kwa wateja wake kuchukua kadi zao za ‘Faida chip and
pin Debit Card’ zilizotambulishwa mapema mwezi Januari mwaka
zilizochukua nafasi ya ‘Magnetic Stripe Faida Debit Card’.
Kadi
za ‘Faida chip and pin Debit Card’ hutoa usalama wa hali ya juu kutokana
na uwepo wa ‘embedded chip’ inayodadavua taarifa za mteja ikiwa na
mfumo madhubuti wa kiusalama hivyo kutoruhusu unakili wa taarifa za
mteja husika.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji wa
Benki ya Exim, Bw. Eugen Masawe jijini Dar es Salaam jana, mwisho wa
kuchukua kadi hizo ni tarehe 15 Aprili, hivyo wateja wamebakiwa na siku
zipatazo 13 kuanzia leo.
“Tunatoa
wito kwa wateja wetu kuchukua kadi zao za ‘Faida chip and pin Debit
Card’ ambazo ni salama zaidi ukilinganisha na ‘Magnetic Stripe Faida
Debit Card’ zilizokuwa zikitumika hapo awali.
“Wateja
hawatakuwa na uwezo wa kutumia kadi zao za zamani kuanzia tarehe 15
Aprili, kwani kadi hizo zitafungiwa. Hivyo wateja wanapaswa kutembelea
matawi yao ili kuchukua kadi mpya,” alisema Bw. Masawe.
Bw.
Masawe alisema kuwa benki yake imedhamiria kutoa huduma bora kwa wateja
na kusisitiza juu ya uchukuaji wa kadi hizo ambazo zitawasaidia wateja
kufanya miamala yao ya kila siku katika mazingira salama zaidi.
“Kwa
kutumia kadi hii mpya ya kimataifa kutoka Benki ya Exim, mteja anaweza
kuwa na uhakika kwamba miamala yake inafanyika katika mazingira salama
kabisa,” alisisitiza.
Aliongeza
kuwa, Kadi hiyo mpya ya kimataifa inamuwezesha mteja kufanya miamala
duniani kote katika mashine za ATM na POS zilizothibitishwa na
MasterCard.

