JUMUIYA
ya wanataaluma wa Chuko Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) jana walifanya
mkutano kuhusu athari za sheria ya takwimu na sheria ya makosa ya
mtandaoni za mwaka 2015 ili kupata maoni mbalimbali juu ya sheria ya
uhuru wa vyombo vya habari.
Mdahalo
huo uliofanyika ukumbi wa Nkrumah wengi wao walichangia juu ya maboresho
ya mswada wa sheria hiyo iliyojadiliwa bungeni kwamba iwapo Rais
Kikwete atasaini sheria hiyo, ni dhahiri itawanyima uhuru na haki za
msingi wanahabari na asasi za raia katika kutoa mchango wake wa utoaji
maoni.
Walimtaka rais asisaini muswada huo.
(PICHA/STORI:DENIS MTIMA/GPL)