Rais wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein anatarajiwa kuwa
mgeni rasmi katika sherehe za uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka
2015 ambazo Kitaifa zinafanyika Mkoani Ruvuma.Kauli hiyo imetolewa leo
na Waizri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara
wakati wa mazoezi ya ya mwisho yaliyofanyika katika Uwanja wa mpira wa
Majimaji mjini Songea.Waziri Fenella amesema kuwa maandalizi yameenda
vizuri na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika sherehe hizo za
uzinduzi wa mbuio za Mwenge na kutoa hamasa zaidi kwa Vijana wotye
nchini kushuhudia uzinduzi huo ata kwa vile utaonyeshwa moja kwa moja
kupitia Televisheni ya Taifa (TBC).
"Nisema
tu kuwa maandalizi yamekwenda vizuri sana mmejionea vijana wa Halaiki
walivyo onyesha umahiri wao, niwatate tu wakazi wa mjini wa Songea
mjitokeze kwa wingi kuja kushuhudia sherehe hizi za uzinduzi wa mbio za
Mwenge wa Uhuru lakini pia VIjana nchini kote shuhudieni tukio hili
muhumu kwa kuwa litaonyeshwa moja kwa moja na Televisheni ya Taifa TBC"
Alisema Dkt.Fenella
Aidha
Waziri Fenella alitoa rai kwa wananchi wa mkoa wa Ruvuma kujitokeza kwa
wingi katika zoezi a kujiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura na
baadaye watumie demokrasia kupiga kura wakati wa uchaguzi mkuu
utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Mbio za
Mwenge wa Uhuru za mwaka 2015 zinazindulia rasmi tarehe 29 Aprili 2015
mkoani Ruvuma na kilele chake kitakuwa tarehe 14 Oktoba mkoani Dodoma
ambapo mbo hizo kwa mwaka huu zimebeba kauli mbiu ya "Tumia Haki yako ya
Kidemokrasia" Jiandikishe na kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka
2015.
Mwenge huo wa Uhuru unatarajiwa kukimbizwa katika halmashauri 168 za mikoa 30 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.