Mkuu
wa Wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema akizungumza na waandishi wa Habari
leo jijini Dar es salaam. Maadhimisho ya mwaka huu yatapambwa na Kauli
Mbiu isemayo Miaka 51 ya Muungano, Tudumishe Amani Na Umoja, Ipigie Kura
ya Ndiyo Katiba inayopendekezwa na Kushiriki Uchaguzi Mkuu.
Askari
watakaoshiriki kwenye Gwaride la heshima litakalohusisha vyombo vya
ulinzi na usalama wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar wakiwa wamebeba bendera za Majeshi ya Tanzania
ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho ya sherehe hizo uwanja wa Uhuru
leo jijini Dar es salaam.
Askari
wa Kikosi Maalum cha Jeshi la Maji wakipita mbele ya jukwaa kuu la
uwanja wa Uhuru kwa mwendo wa kasi ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya
sherehe za miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo jijini Dar
es salaam.
Askari
wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kitengo cha Mawasiliano wakipita mbele
ya jukwaa kuu la uwanja wa Uhuru kwa mwendo wa kasi ikiwa ni sehemu ya
maandalizi ya sherehe za miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
leo jijini Dar es salaam.
Askari
wa Kikosi Maalumu cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (Komando) wakipita
mbele ya jukwaa kuu la uwanja wa Uhuru kwa mwendo wa kasi ikiwa ni
sehemu ya maandalizi ya sherehe za miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar.
Askari
wa Kikosi cha anga wa JWTZ wakipita mbele ya jukwaa kuu la uwanja wa
Uhuru kwa mwendo wa kasi ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya sherehe za
miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. (Picha na Aron Msigwa –
MAELEZO).
Na Aron Msigwa, Msigwa
Serikali
imesema kuwa maandalizi ya Sherehe za Miaka 51 ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar yamekamilika na kwamba sherehe hizo zitafanyika
katika uwanja wa Uhuru Aprili 26 mwaka huu.
Akitoa
ufafanuzi kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya sherehe hizo kwa niaba
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam leo, Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bi. Sophia
Mjema amesema maadhimisho ya mwaka huu yatapambwa na Kauli Mbiu isemayo
Miaka 51 ya Muungano, Tudumishe Amani Na Umoja ,Ipigie Kura ya Ndiyo
Katiba inayopendekezwa na Kushiriki Uchaguzi Mkuu.
Amesema
Tanzania katika kipindi cha miaka 51 ya Muungano imepata mafanikio
makubwa katika Nyanja mbalimbali za maendeleo ya jamii, uchumi,
Siasa,Ulinzi, Usalama na Uhusiano wa Kimataifa.
Bi.
Mjema amefafanua kuwa maadhimisho hayo yataongozwa na Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete ambaye atakuwa mgeni rasmi
na kupambwa na michezo ya Halaiki, ngoma za asili, vikundi vya burudani
na Gwaride la heshima litakalohusisha vyombo vya ulinzi na usalama.
Pia
yatapambwa na Wimbo maalum utakaoimbwa na vijana wa halaiki na ndege
vita za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) zitakazopita mbele ya mgeni
rasmi Kama sehemu ya shamrashamra ya sherehe hizo.
Ametoa
wito kwa wananchi wajitokeze kwa wingi kuhudhuria maadhimisho hayo na
kufafanua kuwa milango ya uwanja wa Uhuru itakuwa wazi kuanzia saa 12:30
asubuhi ili kuwawezesha wananchi kuingia kushuhudia sherehe hizo.
Aidha,
ameutaka uongozi wa SUMATRA na wamiliki wa vyombo vya usafiri
(Daladala) kuelekeza magari yao ya abiria kwenda uwanja wa Uhuru ili
kurahisisha huduma ya usafiri kwa wananchi

