Wiki iliopita ilitolewa takwimu za wachezaji wakali (bora) kwenye
kila idara yaani kuanzia makipa, mabeki, viungo mpaka washambuliaji
mwaka huu 2015 tokea uanze.
Sasa kwenye washambuliaji wakali kwa sasa barani Ulaya, mchezaji bora duniani Cristiano Ronaldo, hakuwepo kwenye 10 bora na wala hakuwepo
kwenye 20 bora. Jamaa amekamata namba 29.
Ajabu kweli kweli, lakini ndio hivyo. Kwa washambuliaji wakali tokea mwaka huu uanze huko barani Ulaya, ni mpinzani mkubwa wa Cristiano, Messiiiiiiiii…., akifuatiwa na Arjen Robben wa Bayern Munich.
Jana kocha wa Real Madrid akakiri kuwa ni kweli mchezaji wake ameshuka kiwango, ila atarudi tena hivi karibuni.
Cristiano amepiga kimya, leo kawajibu watu bana…
Timu yake ya Real Madrid imeshinda 9-1 kwenye La Liga huku yeye akipiga magoli matano peke yake, yakiwemo magoli matatu (hat-trick) ya ndani ya dakika 8.
Kama kawaida ya Cristiano na Messi, wakifunga basi kuna rekodi au takwimu fulani wanakuwa wamefikia au kuvunja na kuweka mpya.
Sasa hebu tucheki magoli hayo matano ya Cristiano yametuletea vitu gani leo…..
1] Hii ni mara ya kwanza kabisa kwa mchezaji huyo kufunga magoli matano tokea ajiunge na Real Madrid na ni hat-trick yake ya upesi zaidi.
2] Ni mchezaji wa kwanza wa Real Madrid kufunga hat-trick ndani ya dakika nane bila penati tokea mwaka 1960. Lakini si kwamba ndie wa kwanza kufunga magoli matano peke yake kwenye klabu hiyo…
3] Sasa amefunga hat-trick ya 24 kwenye La Liga ndani ya misimu sita tokea ajiunge na Real Madrid na kumfikia Lionel Messi. Wote wawili wana hat-trick sawa sasa kwenye Ligi Kuu ya Hispania. Messi amefunga hat-trick zake ndani ya misimu misimu 11.
Wastani wa Cristiano hapa ni mzuri sana. Hii ina maana kuwa kila msimu ana uwezo wa kufunga hat-trick 4, katika miaka sita yake ndani ya Real Madrid, wakati Messi ana wastani wa hat-trick 2 kwa msimu mmoja kwa miaka yake 11 mpaka sasa ndani ya Barcelona.
4] Ndie mchezaji mwenye hat-trick nyingi ndani ya Real Madrid kwenye La Liga.
5] Hat-trick yake ya leo pia imemfanya afikishe hat-trick 28 jumla tokea ajiunge na Real Madrid.
Hii ina maana katika michuano yote aliocheza na timu hiyo.
Na kwa idadi hizo za hat-trick 28, basi leo Cristiano amemfikia mkongwe wa zamani Alfredo Di Stefano wa timu hiyo. Yaani wote wana hat-trick sawa kila mmoja kwenye historia ya klabu hiyo.
Di Stefano ana hat-trick 22 kwenye La Liga, huku 6 nyingine zikiwa kwenye michuano ya Ulaya.
Yeye na Di Stefano ndio wachezaji wenye hat-trick nyingi zaidi kwenye historia ya Real Madrid.
6] Kwa ujumla hiyo ni hat-trick ya 31 kwa mchezaji huyo tokea aanze kucheza soka la kulipwa akiwa na klabu tofauti alizopitia pamoja na timu ya taifa ya Ureno.
7] Mpaka sasa amefunga jumla ya magoli 299 katika mechi 287 alizocheza akiwa amevaa uzi wa Real Madrid.
Rekodi safi kabisa hii. Yaani magoli mengi kuliko idadi ya mechi alizocheza.
8] Ana magoli 36 sasa katika mechi 26 alizocheza msimu huu kwenye Ligi Kuu ya Hispania.
Bado mambo yanakuja… Chukua kwanza hiyo… Nakuja baadae kidogo na list ya wachezaji waliokwishawahi kufunga magoli matano kwenye mechi ndani ya Real Madrid na Ligi Kuu ya Hispania kwa ujumla.