Na: Hassan Hamad, OMKR
Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amezindua
vikundi saba vya mazoezi katika Jimbo la Gando, na kutoa wito kwa
wananchi kufanya mazoezi.
Katika
uzindui huo uliofanyika Skuli ya Kizimbani Wete Pemba, Maalim Seif
amesisitiza kuwa mazoezi ni muhimu katika kujenga afya za wananchi
pamoja na kuimarisha umoja na mshimano miongoni mwao.
Amewahamasisha
wananchi kujijenga katika kufanya mazoezi, kwani ni kinga ya maradhi
mbali mbali, jambo ambalo linaweza kupunguza gharama za matibabu.
Amesema
mazoezi pia yanaibua vipaji vya wanamichezo, na kuahidi kuwa serikali
inaendelea kushirikiana na vikundi vya mazoezi katika kuibua na
kuviendeleza vipaji hivyo.
Amesema
Serikali inatambua umuhimu wa mazoezi, ndio maana Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akatangaza
tarehe mosi Januari ya kila mwaka kuwa siku ya mazoezi Zanzibar.
Katika
kuunga mkono vikundi hivyo vipya, Maalim Seif aliahidi kuchangia
shilingi milioni mbili na laki moja kwa ajili ya vikundi saba
alivyovizindua na kuvikabidhi vyeti kwa kuendelea na mazoezi.
Mapema
akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na
Michezo Mhe. Said Ali Mbarouk, amesema Wizara yake itakuwa mstari wa
mbele kushirikiana na vikundi vya mazoezi nchini.
Uzinduzi huo ulitanguliwa na maandamano ya vikundi kadhaa vya mazoezi kutoka Kisiwani Pemba yalianzia barabara ya Baraza la Wawakilishi Pemba hadi Skuli ya Kizimbani, na baadaye kufanyika mazoeni ya viungo pamoja na mashindano ya kuvuta kamba na mbio za magunia.
Uzinduzi huo ulitanguliwa na maandamano ya vikundi kadhaa vya mazoezi kutoka Kisiwani Pemba yalianzia barabara ya Baraza la Wawakilishi Pemba hadi Skuli ya Kizimbani, na baadaye kufanyika mazoeni ya viungo pamoja na mashindano ya kuvuta kamba na mbio za magunia.

