Na Editha Karlo,
Globu ya Jamii - Kigoma
MKAZI wa Kijiji cha
Buzebazeba katika Manispaa ya Kigoma Ujiji,
Zuwena Abdu (29) jana amejifungua
watoto mapacha wanne kwa mkupuo katika Hospital ya Mkoa wa Kigoma
(Maweni).
Zuwena alisema kuwa
watoto aliojifungua wenye jinsia ya kiume ni watatu na mmoja ambaye
ni wa mwisho ana jinsia ya kike ,wa kwanza akiwa na uzito wa kilo 1.8,pili 2.5
wa tatu 1.7 na wanne 1.7.
Alisema watoto hao
alijifungua jana majira ya saa kumi na mbili jioni salama kwa njia ya
kawaida
Zuwena alisema huo ni
uzazi wake wa tano ambao awali alijifungua wanne kwa njia ya kawaida kwahiyo
jumla anaidadi ya watoto nane.
''Kwanza nina
mshukuru mungu kwa kuniwezesha kujifungua salama watoto wote na wakiwa hai
kutokana na hali duni ya kiuchumi ya familia yetu mimi na mume wangu
tunaomba Watanzania wenye mapenzi mema watusaidie ili tuweze kuwalea hawa
watoto,mume wangu hana kazi na mimi sina kazi''alisema mama huyo
Muuguzi wa zamu
katika wodi ya wazazi Agness Nguvumali alisema kuwa alifikishwa
mama huyo alifikishwa hospitalini hapo siku ya jumatatu saa kumi jioni akiwa na
uchungu na ilipofika saa kumi na mbili akawa amejifungua mapacha wanne kwa njia
ya kawaida salama.
Muuguzi huyo alisema
kuwa watoto wote wana afya njema alisema wataendelea kubaki hospitalini hapo
kwaajili ya uangalizi wa karibu wa madaktari.
Agness amewaomba
Watanzania,mashirika mbalimbali kujitokeza kumsaidia mama huyo ili aweze
kuhudumia watoto wake hao kwakuwa hali yake ya uchumi na mume wake siyo nzuri
na utunzaji wa mapacha hao unahitaji uwezo wa nguvu ya ziada.
YEYOTE MWENYE
MSAADA KWA WATOTO HAO ANAWEZA KUWASILIANA KWA KUTUMIA NAMBA 0752202783
Mama wa watoto
mapacha wanne, Bi. Zuwena Abdu akiwa wodini baada ya kujifungua.
Muuguzi wa zamu
katika Wodi ya wazazi ya Hospital ya Mkoa wa Kigoma (Maweni), Agness Nguvumali
akiwaangalia mapacha wanne waliozaliwa hospitalini hapo.