https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    MWANAMKE MWENYE BUNDUKI AUWAWA UTURUKI AKIVAMIA POLISI

    Mwanamke aliyekuwa na bunduki pamoja na mabomu ya kurusha kwa mkono amepigwa risasi na kufa akijaribu kufanya shambulizi katika makao makuu ya polisi nchini Uturuki, ikiwa siku moja tu kupita baada ya kutokea utekaji katika Jiji la Instabul.

    Picha ya mwanamke huyo mwenye nywele zenye rangi nyekundu akiwa amelala chini, akiwa na bunduki pembeni yake imeonyeshwa kwenye televisheni zinaonyesha polisi wakizingira maeneo ya jirani ya mtaa wa Aksaray.

    Tukio hilo limetokea siku moja baada ya mwendesha mashtaka wa Uturuki, Mehmet Selim Kiraz, kutekwa mahakamani na mtu kundi la Revolutionary People's Liberation Party-Front (DHKP-C) na kisha kuuwawa.
                                 Mtekaji akiwa na mwendesha mashtaka Mehmet Selim Kiraz
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MWANAMKE MWENYE BUNDUKI AUWAWA UTURUKI AKIVAMIA POLISI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top