Mwenyekiti wa ACT-Tanzania, Lucas
Kadawi Limbu (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa
habari Dar es Salaam jana, ambapo alipinga Msajili wa Vyama Siasa
Nchini, Jaji Francis Mtungi kubadilisha jina la chama cha ACT-Tanzania
na kuwa ACT-Wazalendo bila ya kufuata utaratibu. Kulia ni Katibu Muenezi
wa chama hicho, Fredy Kisena na Katibu Mkuu wa chama hicho, Leopold
Mahona.
Viongozi wa chama hicho wakiwa meza
kuu. Kutoka kushoto Kaimu Katibu wa chama hicho, mkoa wa Dar es Salaam,
Peter Katunka, Kaimu Katibu Mkuu, Leopold Mahona, Mwenyekiti, Kadawi
Lucas Limbu na Katibu Muenezi Fredy Kisena.
Mwenyekiti wa ACT-Tanzania, Lucas Kadawi Limbu.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mwenyekiti wa ACT-Tanzania, Lucas Kadawi Limbu (kulia) akisisitiza jambo.
Na Dotto Mwaibale
MWENYEKITI wa Chama cha Alliance for
Change and Transparency (ACT-Tanzania), Lucas Kadawi Limbu amemlalamkia
Msaji wa Vyama vya Siasa Nchini, Jaji Mstaafu Francis Mtungi kwa madai
ya kukiuka utaratibu wa kubadilisha jina la chama hicho na kuwa
ACT-Wazalendo.
Limbu alitoa malalamiko hayo mbele za waandishi wa habari Dar es Salaam jana na kuhoji nyuma ya ACT-Wazalendo kuna nini.
"Tunashangazwa na jaji Mtungi kwa
kubadili jina la chama chetu bila ya kufuata taratibu huku akijua fika
kuna kesi ya msingi ipo mahakama kuhusu mwenendo wa chama hicho. Alisema
Limbu
Aliongeza kuwa kuna njama za makusudi zilizofanywa za kubadilisha jina la chama hicho kwani haiwezeka na haiingii akilini kubadilisha jina la chama kwa kipindi kifupi na haraka kiasi hicho.
"ACT-Tanzania ni chama chetu sio cha Zitto na kama anahitahi siasa safi aanzishe chama chake kwani nafasi hiyo ipo wazi kwa kila mtanzania.
Alisema ni jambo la ajabu kuona chama kinafanya mkutano wake mkuu wenye nia hofu na kumpatia mtu madaraka ya kioongozi mkuu na kubadilisha jina lake huku msajili wa vyama akishuhudia.
Alisema msajili wa vyama vya siasa alitoa tamko la kubadilishwa jina la chama hicho tarehe 20-4-2015 wakati tayari kiongozi mkuu wa chama hicho kilichobadilishwa jina akiwa katika zaira ya kichama mikoani aliyoianza tarehe 10-4-2015 huku wakigawa kadi kwa kupitia chama cha ATC-Wazalendo.
Limbu alihoji fedha zinazotumika kwenye ziara hiyo na za kuchapa kadi, bendera za chama na vifaa vingine kuwa zinatoka wapi kama hakuna watu wenye nia mbaya na chama cha ATC-Tanzania. (Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habarizajamii.com/)