Meneja wa Utafiti na Maendeleo wa NHBRA Injinia Elias
Kwemana akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa habari MAELEZO
Ajijini Dar es Salaam leo kushoto ni kaimu afisa Habari wa NHBRA Frimin Lyakurwa
kulia ni Afisa masoko wa NHBRA Zubeda Salum.
Meneja wa Utafiti na Maendeleo wa NHBRA
Injinia Elias Kwemana akionyesha aina ya
kwanza ya kigae cha kupaulia nyumba,kushoto ni kaimu afisa Habari wa NHBRA Frimin Lyakurwa
kulia ni Afisa masoko wa NHBRA Zubeda Salum.
Meneja wa Utafiti na Maendeleo wa NHBRA Injinia
Elias Kwemana akionyesha aina ya pili ya
kigae cha kupaulia nyumba,kushoto ni kaimu afisa Habari wa NHBRA Frimin Lyakurwa.
Baadhi ya wandishi wa habari waliohudhuria
katika mkutano wa kuonyesha aina mbalimbali za vigae vinavyoweza kutengenezwa
na kila mwananchi hapa nchini katika ukumbi wa Habari MAELEZO jijini Dar es
Salaam. (PICHA ZOTE NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII)
Na Avila
Kakingo,Globu ya Jami.
WAKALA Taifa
wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) wamegundua njia rahisi ya
kuboresha makazi kwa kutumia vigae kwa gharama nafuu ambazo kila mwananchi anaweza
kuzimudu.
Hayo
yamesemwa na Meneja wa Utafiti na Maendeleo wa NHBRA Injinia Elias
Kwemana akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa habari MAELEZO jijini
Dar es Salaam leo. Kwemana amesema kuwa utengenezaji wa vigae
hivyo ni rahisi na gharama hafuu kwani bidhaa zote za kutengeneza vigae hivyo zinapatikana
hapa hapa nchini.
Hifaa
hivyo vinavyotumika kutengenezea vigae hivyo ni
mchanga sementi na nyuzi za katani
bidhaa hizo zote zinapatikana hapahapa
nchini, ikiwa kuna mashine inayotumika kushindilia mchanga
uliochanganywa na sementi nayo ni gharama nafuu ukilinganisha na faida
zinazopatikana.
Kwemana
amesema kuwa njia ya kutengeneza vigae
hivyo vitasaidia kutumika kama njia
nyingine ya kupaua nyumba zetu ambapo vigae hivyo huu kaa muda mrefu kuliko kutumia Nyasi au Bati.





