Ifuatayo ni hotuba ya Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe Ali Hassan Mwinyi alipohutubia mkutano wa nne wa Chama cha Ukuzaji
Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) uliofanyika tarehe 23 Aprili 2015 katika
Chuo Kikuu Cha Howard jijini Washington DC
KARIBU
SHEREHE YA CHAUKIDU YA MCHANA CHUO CHA HOWARD YAFANA KARIBU
Rais
wa CHAUKIDU Prof Lioba Moshi watatu toka kushoto akimkaribisha Rais
mstaafu Ali Hassan Mwinyi mara tu alipowasili kama mgeni rasmi chuo
kikuu cha Howard Washington, DC katika sherehe ya chama cha ukuzaji wa
Kiswahili Duniani siku ya Alhamisi April 23, 2015 kulia ni Prof Venessa
White Jackson
Rais
mstaafu Ali Hassan Mwinyi akimtambulisha mkewe mama Sitti Mwinyi kwa
mwenyeji wao Prof Lioba Moshi pia na yeye akimtambulisha mama Sitti
Mwinyi kwa Prof Venessa White Jackson kushoto ni Balozi wa Tanzania
nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula . 
Prof
Lioba Moshi Rais CHAUKIDU akielezea historia fupi ya CHAUKIDU na baadae
kumkaribisha Rais mstaafu kuongea na wadau wa Kiswahili waliohudhuria
sherehe ya chama hicho iliyofanyika siku ya Alhamisi April 23, 2015
katika chuo kikuu cha Howard kilichopo Washington, DC.
Ms
Mamburi Lyambaya (kushoto) akimtambulisha Prof Venessa White Jackon na
yeye kuwasalimia wadau wa Kiswahili waliohudhuria sherehe ya CHAUKIDU
iliyofanyika katika chuo kikuu cha Howard Washington, DC.
Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akiwa meza kuu kulia ni prof Venessa White Jackson '
Rais
mstaafu Ali Hassan Mwinyi akitoa hotuba kwa kuwashukuru CHAUKIDU kwa
kummpa mwaliko na kwa kuwa yeye ni mdau mkubwa wa lugha ya Kiswahili
hakusita kukubali kuja kujumuika nao pia Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi
aliwapongeza kwa kuitangaza lugha ya Kiswahili nchini Marekani.
Kutoka
kushoto ni Balozi wa Umoja wa Afrika Mhe. Amina Salum Ali, Balozi wa
Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula na mama Sitti Mwinyi
wakifuatilia hotuba ya Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi.
Wanafunzi
wa chuo kikuu cha Howard wakiimba nyimbo za Kiswahili kwa ustadi mkubwa
kuliko wastajabisha Watanzania na wadau wengine wa Kiswahili.
Wadau wa Kiswahili wakifuatilia sherehe ya CHAUKIDU
Asha
Nyang.anyi akiwa kwenye meza akikagua majina ya wadau wa Kiswahili
kwenye sherehe ya Chama Cha Ukuzaji Wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU)
inayoendelea sasa hizi chuo kikuu cha Howard kilichopo Washington, DC na
Rais msataafu Ali Hassan Mwinyi atakua mgeni rasmi.
Wadau wa Kiswahili wakiendelea kuingia ukumbini.
Wadau kutoka Zanzibar wakipata picha
Walimu wa kiswahili wa vyuo mbalimbali wakipata picha ya pamoja.
wadau wa Kiswahili wakihudhuria sherehe ya CHAUKIDU
Walimu
na maporofesa wa vyuo wakiwa ndani ukumbi wa Blackburn Center siku ya
Alhamisi April 23, 2015 chuo kikuu cha Howard kilichopo Washington, DC.
Wadau wa Kiswahili wakibadilishana mawili matatu.
Wadau wa Kiswahili wakilonga Picha zaidi Baadae

.jpg)
